Sunday, November 27, 2011

Nape akutana na wana CCM na watanzania Houston

Katibu wa Itikadi na Uenezi - CCM Taifa Mh. Nape Nnauye akiongea na wanachama wa CCM Tawi la Marekani na watanzania waishio nchini humo huko Houston Texas. Katika ziara hiyo Mh aliaambatana na Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi Ndugu Sixtus Mapunda. Katika mkutano ambao ulifanyika katika ukumbi wa Swiss Royale, Houston. Mh Nape alielezea dhana nzima ya mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo maarufu kama 'kujivua gamba'. Alieleza kuwa kujivua gamba ni muhimu kwa sasa hivi ili kukipa chama sura mpya na mvuto kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla. CCM ni moja kati ya vyama vinne duniani vya kisiasa na kidemokrasia ambavyo vimekuwa madarakani kwa ridhaa ya wananchi kwa muda mrefu, kwa maana hiyo chama makini ni lazima kiendane na wakati ili kiweze kuendelea kupata ridhaa zaidi ya kuongoza. Mh nape aliongeza kwamba, ili chama kipate kasi zaidi ya kutumikia wananchi na kuisimamia serikali yake iliyopo madarakani, Chama Cha Mapinduzi kinajijenga zaidi ndani kwenye Idara zake ili ziweze kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadae.
Aidha Mh Nape aliwaasa wana CCM kuwa imara na kuhakikisha kuwa chama kinapata nguvu na mafanikio zaidi na zaidi. Akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa waliohudhuria, Mh Nape alisisitiza kuwa CCM Marekani haina mgogoro wowote wa uongozi na kuwasihi wanachama kutoa ushirikiano kwa viongozi halali wa tawi waliochaguliwa kikatiba.
Kabla ya kumkaribisha Mh Nape, Mwenyekiti wa watanzania waishio Houston Bw. Novatus Simba alimshukuru Mh Nape na ujumbe wake kwa kuweza kufika Houston na kubadilishana mawazo na uzoefu juu ya mambo mbalimbali hasa yale yanayotokea huko nyumbani Tanzania. Bw. Simba, alimwomba Mh. Nape kuwa mara kwa mara apatapo nafasi ya kufika Marekani basi anakaribishwa sana kuzuru Houston na kuongea na watanzania juu ya masuala na mustakabali wa mambo kadhaa yanayotokea huko nyumbani.

No comments: