Friday, January 1, 2010

MZEE RASHID MFAUME KAWAWA AAGA ! KINGUNGE AELEZEA WASIFU WAKE

Tanzania imetangaza maombolezo ya siku saba kufuatia kifo cha mmoja wa waasisi wa chama tawala cha CCM,mzee Rashidi Mfaume Kawawa ambaye alikuwa miongoni mwa waliopigania uhuru wa nchi hiyo Kawawa alikuwa mshirika wa karibu wa baba wa taifa hilo Mwalimu Julius Nyerere na aliwahi kushika wadhifa wa waziri mkuu na makamu wa rais wa Tanzania katika utawala wa Mwalimu Nyerere. Pia aliwahi kuwa katibu mkuu wa CCM kabla ya kustaafu.

Kwa mujibu wa mahojiano ya Sauti ya Amerika mmoja na mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini humo Kingunge Ngombale Mwiru alisema kuwa Mzee Kawawa atakumbukwa kama Simba wa Vita kwa kutetea uhuru wa taifa hilo na pia aliunda shirikisho la Wafanyakazi Tanganyika 1955 ambalo lilishirikiana na TANU katika kutafuta uhuru wa nchi hiyo upande mmoja na kwa upande mwingine haki za wafanyakazi, aliongeza kuwa atakumbukwa kama mchapa kazi na mwaminifu alikuwa waziri mkuu 1962 kwa kuwa Mwl. Nyerere aliamini kuwa ni mtu mwaminifu mchapakakazi na mwenye uwezo wa kuongoza wenzake.

Atakumbukwa kwa kazi ya kujenga taifa jipya akiwa waziri mkuu na baada ya muungano akawa makamu wa pili wa Rais, alishughulikia ulinzi na Vijana na pia kuanzishwa kwa jeshi la wananchi na jeshi la kujenga taifa.

Mwishoni mwa maisha yake alikuwa mshauri mkubwa na mlezi wa Taifa ameonyesha uzalendo na unyeyekevu na hana makuu kazi yake ilikuwa kutumikia watu na ndio maana vijana wa CCM walimteuwa kuwa kamanda wao mlezi wao mkuu.

Alizaliwa Songea mwaka 1926. Alipata elimu ya msingi huko Songea na baadae jijini Dar-es-salaam. Alijiunga na masomo ya sekondari huko Tabora mwaka 1951-1956. Kawawa alikataa nafasi ya kuendelea na masomo ya juu katika chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda ili kuweka bidii zake katika harakati za kugombania uhuru wa Tanganyika.

No comments: