skip to main |
skip to sidebar
Rais Kikwete awasili nchini Msumbiji
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtoto Queen Kinguti(9) muda mfupi baada ya kuwasili jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Armando Guebuza kuendelea na muhula wa pili wa urais baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Oktoba Mwaka jana.Queen ambaye wazazi wake ni wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji alikuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kumlaki Rais Kikwete na mkewe Mama Salma jana jioni.
Mtoto Queen Kinguti(kushoto) na Mwenzake Khalid Mgidos(kulia) wakiwakaribisha kwa maua Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Armando Guebuza kuendelea na muhula wa pili wa uraisMsomajiMsumbiji
No comments:
Post a Comment