Sunday, December 21, 2008

UKAIDI HUU SI WAKUVUMILIWA.

Huu ni upande wa mbele wa kiwanda cha Brookside kilichopo Arusha - Tanzania kinachodaiwa kuwa ni cha kusindika maziwa, hata hivyo habari za kuaminika zinasema kwamba kiwanda hiki si cha kusindika maziwa na kwamba kimekuwa na kawaida ya kukusanya maziwa na kuyapeleka Kenya ili yasindikwe na kisha kuyarudisha Tanzania ili kuyatafutia masoko. Hivi karibuni waziri wa viwanda na biashara Dr. Mary Nagu alikipiga marufuku kiwanda hicho kwa madai hayo hayo hata hivyo agizo hilo lilipuuzwa kwa kile kilielezwa kwamba serikali ya Tanzania haiwezi kufanya chochote kwa kuwa kiwanda hicho kinamilikiwa na familia ya rais wa zamani wa Kenya Bw. Jomo Kenyatta. Mama Nagu upo?

Ndejembi Michael.

9 comments:

Anonymous said...

Lengho hasa la wawekezaji ni nini?.

Tanzania inabidi tuwe makini na mambo tunayo yafanya.

Anonymous said...

Hiki kiwanda poa sana kama kingefanya kazi inavyotakiwa katika mikataba.

Anonymous said...

Hawa ndio wale wewekezaji wanaokuja na masharti magumu. Hata waziri haruhusiwi kuwagusa. Kweli kazi zingine mimi sitokaa nifanye kama mambo yenyewe ndio hivi

Anonymous said...

Unaweza kukuta nao wana bailout kutoka kwenye serikari za nchi zao. Hii kali

Anonymous said...

Kwahiyo hata waziri ana final say, hiyo kali. Mambo ya uwekezaji uliosainiwa chini ya 10 %. Kweli bongo kazi hipo.

Anonymous said...

Hivi unajua uchumi wa kenya umeshikiliwa na watu wachache sana na mtu wa kawaida athaminiwi hata kidogo. Sasa na sisi tuwe makini nao sio waje kwetu natabia zao za kishenzi. watanzania wenzagu inakuwaje tunafanyiwa ushenzi na sisi tunakubali.

Anonymous said...

Hiki kiwanda kweli kinamilikiwa na mkenya maana hata langi na bendera ndio hizo za kwao. Unajua wenzetu ukabila umewatawala na ndio maana hata wanapokuja kwetu bado wanataka kuleta hule ushenzi wao wa kikabila. Nashukuru sana ndugu ndejembi kwa mada hii.

Pia nawapogeza, hii site yenu inamambo mbali mabali ya maana sio tu umbea.

mwana chama ccm

Anonymous said...

Wakenya hatuwaitaji nchini kwetu. Mh. waziri maamuzi yako yalikuwa sawa kabisa maana hawa watu hawatufai hata kidogo.

Anonymous said...

Wawekezaji wa kenya kweli masharti yao yatakuwa ni magumu kwasababu hizo bendera zenyewe sioni hata moja inayowakilisha Tanzania