Friday, December 19, 2008

KIKWETE AWAGEUKIA ATCL

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete amerishutumu vikali shirika la ndege Tanzania (ATCL) kwa uzembe uliopelekea shirika hilo kufungiwa, na pia amemtaka waziri wa miundo mbinu Mh. Shukuru Kawambwa kukutana na menejiment ya shirika hilo ili kutatua tatizo hilo

Msomaji wetu.

9 comments:

Anonymous said...

Kweli kuongoza nchi yetu si mchezo. Sasa hawa jamaa wanataka tuwe tunatembe kwa miguu, au ?

Anonymous said...

Kweli tanzania safari bado ni ndefu, inakuwaje tunamfanyisha kazi rais wetu kiasi hiki. Rais fukuza uongozi mzima, maana kuna vijana wengi wanamaliza shule na awana kazi. Tusikalie tu mambo ya watu wengine wanauzoefu kumbe sio wabunifu. Pia napendekeza wakurugenzi wawe wanatoa report kila baada ya miezi sita,kama report si nzuri kazi kwisha.

Dar

Anonymous said...

Hawa wamezidi bwana kwa nini asiwatimue tu? mi ningeshauri awatimue wote tu maana wanaonyesha kutokujali ile hali ndugu zetu wanahitaji usfiri wa anga.

Israel

Anonymous said...

mabisho hao hawana loolote jk timua wote, hatutaki maelezo wala nini.

houston-texas

Anonymous said...

Ndio maana nasema tuliomaliza shule turudi nyumbani, sasa hawa watu kazi imewashinda lakini hawatafukuzwa kwa sababu hakuna watu wa kuwa replace


united kingdom

Anonymous said...

jamaaani nchi yetu inaliwa sana! hawa watu wasiachwe lazima wafukukuzwe na mahakamani wafikishwe kisha segerea.
huu ndio msimamo wetu watanzania tunaoishi huku moscow urusi ya zamani

Anonymous said...

Hao jamaa ni keko tu kama wale wezi wa miepa.

Anonymous said...

jamani, jamani, jamani tanzania yangu, hivi nyi watu hamna huruma hata kidogo ee? yaani mpaka mtaji mnakula? ona sasa shirika limefungwaa.
kikwete timua wote halafu niite mimi nije kuongoza mtaona mambo.

king-south africa

Anonymous said...

Shirika la ndege la nchi limefungwa na huyo,kesho utasikia mkurugenza wa shirika hio hilo ameteuliwa kuongoza shirika lingine. Unajua inasikitisha sana ukifatilia jinsi mambo ya nchi yetu yanavyoendeshwa.