Ndugu wanajumuia,
Uongozi na wana chama wa chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Marekani wanapenda kuwatakia kila la kheri wanajumuia wa Houston katika uchaguzi wa viongozi wa jumuia hiyo hapo jumapili ya Dec 14/ 08 katika ukumbi wa safari hall.
Chama kinaamini kuwa uchanguzi huo utakuwa wa haki na kwamba kila aliye na haki ya kuchagua na kuchaguliwa atapata nafasi hiyo bila mizengwe wala usumbufu usio wa lazima na hasa ikizingatiwa kwamba kamati ya uchaguzi huo iko makini na inatambua wajibu wake huo.
CCM inaamini kuwa wanajumuia wanatambua yakwamba hii ni nafasi pekee kwao kuamua nani wa kuwaongoza kwa maendeleo yao na mustakabali wa jumuia nzima.
Aidha chama kinawakumbusha wanajumuia kukumbuka nafasi kwa akina mama pia ambao ni sehemu ya jumuia yetu, ili waweze kuonyesha uwezo wao katika oungozi kwani ni ukweli usipingika kwamba uwezo, sababu na nia za kuongoza wanazo.
Mwisho, tunawataka watakaochaguliwa kuwa tayari kutimiza ndoto za wanajumuia.
Ndejembi,
M/kiti.
Friday, December 12, 2008
Houston ,Texas-kila la kheri katika uchaguzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Kumbe ninyi ni watu safi eeeh au ni kwa sababu hamja kabidhiwa mifuko ya epa!Ki aina mnanifanya niwaone tofauti na wale mifisadi ya bongo. sisi wa Itali tunafarijika sana kuona viongozi wa CCM wakijumuika na kushiriki ktk kazi za jumuia kama ninyi wa huko marekani mnavyofanya. Jiepusheni na mifisadi ya bongo
Viongozi mtakaochaguliwa tunaomba mzingatie ujumbe huu uliotolewa na hawa wenzetu wa CCM. Tunashukuru sana kwa ujumbe huu ndugu mwenyekiti.
Leo ndio leo, lazima tuwe na uongozi wa nguvu. Na mimi naungana na wenzetu wa CCM kutoa salaam kwa wanajumuhia. Ndugu mwenyekiti, nipatie basi hiyo card ya CCM nikapambane na hao mafisadi.
Post a Comment