Thursday, February 23, 2012

MH NAPE AELEZEA MABADILIKO YA KATIBA YA CCM



CHAMA Cha Mapinduzi kimefanya mabadiliko ya Katiba yake ya mwaka 1977 toleo la 2010 na kanuni zake, baada ya Halmashauri kuu ya chama hicho chini ya Mwenyekiti wake wa taifa Rais Jakaya Kikwete.Mabadiliko ya katiba ya CCM. Akielezea mabadiliko hayo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye anasema, kwanza Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imebadili namna ambavyo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inavyopatikana.“Wajumbe hao waliokuwa wakipatikana kutoka kwenye ngazi ya mikoa, sasa wamegawanywa katika makundi sita ambayo ni ngazi ya Taifa itakayokuwa na wajumbe 10 kutoka Tanzania Bara na wajumbe 10 kutoka Tanzania visiwani” anasema na kuongeza, “Kundi la pili litahusisha wajumbe 10 wa kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM Taifa. Kundi la tatu linahusisha wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao wakati kundi la nne lina wajumbe wanaotoka kwenye vyombo vya uwakilishi kama vile wanaochaguliwa na Bunge nafasi 10 (Bara nafasi nane, Zanzibar nafasi mbili), wanaochaguliwa, Bara tano na Zanzibar nafasi tano)”. Analitaja kundi la tano linalohusisha wajumbe wanaochaguliwa kutoka wilayani nafasi 221. Wajumbe hao waliochaguliwa kupitia wilaya watakuwa ni viongozi wa kazi za muda wote ili kuweka wazi zaidi wajibu wa wajumbe hao wa kuwa karibu na wanachama na kushughulikia shida zao.Kundi la mwisho ni wajumbe toka kwenye jumuiya za chama, kama vile wanaochaguliwa na Umoja wa Wanawake nafasi 15 (Bara nafasi tisa na Zanzibar nafasi sita). “Umoja wa Vijana (UVCCM) nafasi 10 (Bara nafasi sita na Zanzibar nafasi nne). Jumuiya ya Wazazi nafasi tano(Bara nafasi tatu na Zanzibar nafasi mbili)”. Baraza la UshauriKatika mabadiliko hayo Halmashauri kuu ya Taifa imeamua kuwa viongozi wakuu wastaafu ngazi ya taifa waundiwe baraza la ushauri.Nape amesema kuwa, Baraza hilo litakuwa na wajumbe kama vile Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walikuwa wenyeviti wa CCM Taifa. Anawataja wengine kuwa ni pamoja na Marais wastaafu wa Zanzibar ambao pia walikuwa Makamu wenyeviti wa CCM Taifa na Makamu wa mwenyekiti wa CCM Taifa wastaafu.“Baraza litakuwa na kazi ya kutoa ushauri kwa Chama na serikali zinazoongozwa na CCM, kwa madhumuni hayo hayo katika jambo mahsusi. Wajumbe wa baraza hilo wanaweza pia kualikwa ama wote au mwakilishi wao kuhudhuria vikao vya chama ngazi ya Taifa” anasema Nape.

No comments: