Saturday, January 30, 2010

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KAULI YA CCM KUHUSU KUANZISHWA KWA
CHAMA KIPYA CHA UPINZANI – CCJ

Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vinaandika sana habari za kuanzishwa kwa Chamakipya cha upinzani kiitwacho Chama cha Jamii (CCJ). Habari kuhusu ujio wa chama hiki zimekuwa zinapambwa na vibwagizo vingi kwamba kimenzishwa na vigogo wa CCM kwa lengo la kukisambaratisha Chama cha Mapinduzi. Baadhi ya vyombo vya habari na hasa makala katika magazeti yamekuwa yanatabiri na kutarajia kumeguka kwa CCM kutokana na kuanzishwa kwa CCJ.

Chama cha Mapinduzi kinapenda kuwaarifu WanaCCM na Watanzania kwa jumla kwamba.

Kwanza, Chama cha Mapinduzi ndicho kiliruhusu uanzishwe mfumo wa vyama vingi 1992; hii ilikuwa baada ya Watanzania 80% kutoa maoni kwamba mfumo wa chama kimoja (yaani CCM) uendelee, na 20% walitaka uanzishwe mfumo wa vyama vingi. CCM ilikuwa na sababu nzuri ya kuwasikiliza waliowengi (80%), yaani wengi wape!

Lakini kwa kutumia busara kubwa CCM ilitoa fursa ya Watanzania 20% waanzishe vyama vyao vya upinzani na wamekuwa wanavianzisha, hadi sasa vipo 17. Hivyo kuanzishwa kwa chama kipya cha upinzani cha 18 si jambo la ajabu; lakini magazeti yanalikuza mno jambo hili kwa lengo la kuuza magazeti yao na pia kuwatisha Watanzania na hasa WanaCCM kwamba CCM inameguka. Hila hizi ovu hazitofanikiwa!

Pili, Chama hicho kinachoandikwa sana magazetini ndio kwanza kimeomba usajili. Hakijasajiliwa; na inawezekana kisipate usajili kabisa. Kwa mujibu wa sheria chama kinachoomba usajili, kwanza hupata usajili wa muda, na kisha huchukua miezi sita kupata usajili wa kudumu iwapo kitatimiza masharti na vigezo vya usajili wa kudumu. CCJ hawajapata hata usajili wa muda! Kwa kuwa mchakato wa uteuzi wa wagombea utaanza mara tu Bunge litakapovunjwa mwezi Julai, hao vigogo wa CCM watakao hama na kujiunga na CCJ wataomba uteuzi kupitia CCJ wakati gani? Hivyo taarifa kwamba kuna vigogo wengi wa CCM watagombea kupitia CCJ ni uvumi usio na mantiki yoyote. Hakuna kiongozi makini wa CCM atagombea Ubunge au Urais kupitia Chama kisicho na usajili; ni sawa na kuingia katika boti iliyotoboka na kutaka kusafiri nayo baharini!

Tatu, Hata kama ikitokea miujiza CCJ ikapata usajili wa kudumu kabla ya miezi sita na kuingia katika uchaguzi, na hata ikitokea baadhi ya viongozi wa CCM wakaamua kuhama CCM na kugombea kupitia CCJ, halitakuwa tukio la kwanza, wala sio jambo la ajabu. Tukio kama hilo limetokea mara nyingi. Wapo viongozi wengi wa vyama vya upinzani ambao walikuwa viongozi wakubwa CCM; waliamua kuhama, lakini CCM iliendelea kuwepo na iliendelea kuwa imara. Utabiri kwamba baadhi ya vigogo wa CCM wakihamia CCJ utakuwa ndio mwisho wa CCM, unapingwa na historia. Ukweli ni kwamba viongozi waliohama CCM na kwenda upinzani hawakupata mafanikio yoyote huko walikokwenda, wakati CCM waliodhani ingetetereka inaendelea kuwa imara, haijameguka wala kutetereka. Vivyo hivyo ikitokea baadhi ya viongozi wa CCM wakihama na kwenda CCJ au chama chochote cha upinzani, ukweli wa historia utabaki pale pale kwamba CCM itabaki imara, haitameguka wala kusambaratika; bali wao watakuwa wamejimaliza kisiasa. Ni muhimu Watanzania waelewe kwamba umaarufu wa viongozi wa CCM unatokana na umaarufu wa CCM, kiongozi anayeondoka CCM umaarufu wake huporomoka. Huu ndio ukweli wa kihistoria.

Nne, CCM inapenda kusisitiza kwamba wale wote wanaosubiri CCM imeguke wanapoteza muda wao. CCM ina historia ndefu na iliyotukuka, ina mtandao mpana sana, pia inajeshi kubwa la wanachama milioni nne na nusu. Sera za CCM za kupigania haki za wanyonge kuhusu elimu, afya, maji, uwezeshaji wananchi kiuchumi; ujenzi wa barabara za Vijijini na barabara kuu, n.k, zinawavutia watu wengi. Na jambo la muhimu ni kwamba zinatekelezwa vizuri pamoja na maneno ya ghiriba yanayoandikwa katika vyombo vya habari kwamba eti Rais Kikwete na CCM hawajafanya lolote! Hii ni ghiriba ambayo nayo haitafanikiwa. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita ambapo CCM ilipata ushindi wa 91% ni majibu tosha kwa wale wote wenye ndoto mbaya dhidi ya CCM. Matokeo haya ni salamu na ujumbe mzito kwamba wananchi Mijini na Vijijini wanaridhika na Sera za CCM na utekelezaji ilani ya CCM chini ya jemedari Rais Kikwete. Na ni hao hao wananchi watakaopiga kura katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu, na hapana shaka matokeo yatakuwa hayo hayo kwa CCM kuibuka na ushindi mkubwa. Katika mazingira haya ya Chama cha Mapinduzi kukubalika na kuheshimiwa na Watanzania, suala la kumeguka au kusambaratika ni ndoto ya mchana!

Tano, kwa kifupi CCM inapenda kuwatahadharisha WanaCCM kwamba wasitishike na ripoti za magazeti yanayokipamba chama ambacho hakina usajili, chama ambacho hakitashiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao, wala hakuna kigogo hata mmoja wa CCM ambaye hadi sasa aliyejitambulisha kuwa ni mwanachama wa chama hicho. Kelele ni kubwa za kukipamba chama hiki (CCJ) kuliko hali halisi. Vitisho kwamba CCM itameguka ni vingi lakini ni uzushi mtupu. Hizi ni njama na ghiliba; hivyo WanaCCM na wananchi kwa jumla zipuuzeni. CCM ndiyo iliyoanzisha mfumo wa vyama vingi 1992 na hivi sasa vipo 17, haitishiki na hakijapata kutishika na mfumo wa vyama vingi; iweje hicho cha 18 ndicho kiinyime usingizi CCM! Tunatoa wito kwa WanaCCM kwamba tuendelee kujenga chama chetu, tuendelee kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa bidii. Chama cha CCJ ni chui wa karatasi, kisiwahangaishe, ni njama za kutufanya tuchelewe kutekeleza agenda muhimu za chama chetu na tubaki tunafuatilia chama ambacho bado hakina usajili na wala hakitashiriki katika uchaguzi. Tusiingie katika mtego huu uliowekwa na watu wasiokitakia mema chama chetu.

Mwisho kabisa tunapenda kuwahakikishia watanzania kwamba CCM hakikuogopa kuruhusu mfumo wa vyamba vingi, CCM ndiye mwasisi na mkunga wa mfumo wa vyama vingi, hivyo uanzishwaji wa chama chochote cha upinzani haliwezi kuwa tishio kwa CCM. Aidha kwa viongozi wa CCM kuhamia vyama vya upinzani sio jambo jipya na halijaathiri umaarufu na uimara wa CCM. Na mara nyingi viongozi wa CCM wanaohamia upinzani wamekuwa wanarejea CCM baada ya kugundua kwamba kwenye vyama vya upinzani hakuna lolote la maana, na CCM tumekuwa tunawapokea na tutaendelea kuwapokea bila ya kinyongo. Kwa jumla tunawaomba WanaCCM wasitishwe na ghiriba za magazeti kwani chama chetu bado ni imara na tumaini na nguzo ya Watanzania katika kudumisha umoja na amani ya nchi yetu.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na
CAPT JOHN Z. CHILIGATI (MB)
KATIBU WA NEC: ITIKADI NA UENEZI

Wednesday, January 20, 2010

Bunge la Namibia laitembelea benki ya wanawake Tanzania

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mhe. Lucy Nkya akimpa vitabu mbalimbali kuhusu Maendeleo ya Jinsia na Wanawake kiongozi wa msafara wa wawakilishi wa Bunge la Namibia bw. Elia George Kayama
Mkuu wa Msafara wa wawakilishi wa Bunge la Namibia Mhe. Elia George Kayama akipata huduma za Kibenki katika Benki ya Wanawake

Wawakilishi wa Bunge la Namibia na Wajumbe a Kamati ya Maendeleo ya Jamii katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea benki hiyo.

Msomaji
Dar es salaam

Tuesday, January 19, 2010

Rais Kikwete afungua daraja la Mto Simiyu na Kuzindua mradi wa maji wilayani Meatu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria kufungu rasmi daraja la Mto Simiyu,lililopo kati ya mpaka wa wilaya za Bariadi na Meatu,mkoa wa Shinyanga jana
Mbunge wa Bariadi Mashariki John Momose Cheyo(kulia), Mbunge wa Kisesa Mh.Luhaga Mpina (kushoto pembeni ya Rais) pamoja na viongozi wengine wa vyama vya siasa na serikali wakishangilia mara baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua rasmi daraja la mto Simiyu lililopo katika mpaka wa wilaya za Meatu na Bariadi mkoani Shinyanga jana mchana.Wanne kushoto ni Mama Salma Kikwete.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtwika maji Bi.Amina Ramadhani Mkazi wa kata ya Mwanuzi,wilayani Meatu, muda mfupi bada ya kuzindua mradi wa maji wa wilaya ya Meatu,mkoa wa Shinyanga.Kulia nia Waziri wa maji na umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya na watatu kushoto ni Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wakazi wa kata ya Mwandoya wilayani Bariadi jana mchana.
Msomaji
Shinyanga

WAZIRI WA MAMBO YA NCHI ZA NJE MHE.BERNAD MEMBE AFUNGUA MKUTANO WA DIASPORA JIJINI DAR ES SALAA,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akifungua mkutano wa wadau wa majadiliano baina ya wataalamu wa hapa nyumbani na wa nje jijini leo kuhusu uwezekano wa kuwashirikisha kikamilifu Watanzania walio nje ya nchi mkutano huo unaratibiwa na Wizara ya Nje ambayo tayari wameshaunda Idara ya DIASPORA.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Wakimataifa Bernard Membe (KUSHOTO) akiongea katika mkutano wa majadiliano baina ya wataalamu mbalimbali wa hapa nyumbani na wa nje jijini leo kuhusu uwezekano wa kuwashirikisha watanzania walioko nje kurudi na kuwekeza hapa nchini, Pichani mwingine ni Kiongozi wa shirika la kimataifa linaloshughulikia masula ya uhamiaji nchini (IOM- International Organizaion for Migration ) Mr.Par Liljert..
Baadhi ya wadau walioshiriki katika mkutano wa majadiliano ya wataalamu mbalimbali wa hapa na wa nje jijini leo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (hayupo Pichani ) wakati alipofungua mkutano wa majadiliano.
Msomaji
Dar es salaam

Miaka 30 ya huduma za Posta yaadhimishwa jijini Arusha

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akizindua mfumo wa anwani za nyumba na Mitaa Kitaifa katika eneo la Posta Kuu Mjini Arusha ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 30 ya huduma za Posta Barani Afrika. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msola
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akionyeshwa kifaa ambacho kinaweka kumbukumbu za wshitiri wa anwani za nyumba na Mitaa na toka kwa muuzaji wa wakala wa kampuni ya ESCHER GROUP ya Ireland bwana Khalid Sadiki wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya huduma za Posta mjini Arusha.Wengine ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi, naTeknolojia Profesa Peter Msola na Waziri wa Habari,Michezo na utamaduni George Mkuchika.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akijadilia jambo na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia,muda mfupi kabla Dk Shein hajafungua rasmi kongamano na maonesho ya huduma za Posta Barani Afrika kutimiza miaka 30 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC)

Msomaji
Arusha

Mkataba wa mifugo na uvuvi kati ya China na Tanzania

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wa Tanzania John Magufuli ( kulia) akibadilishana hati na Waziri wa Kilimo wa China NIU DUN jijini jana katika sherehe ya kuwekeana saini mkataba wa makubaliano ya Mifugo na Uvuvi kati ya nchi za Tanzania na China

Msomaji
Dar es salaam

Monday, January 18, 2010

Jamali Msellem ajiunga tena CCM kutoka CUF !!

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Jamali Msellem alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi baada ya kujiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi, alipokelewa na Katibu Mkuu CCM, Mhe Yusuf Makamba.

Msomaji
Dar es salaam

KAMATI YA BUNGE YAJADILI MAENEO YA MABADILIKO KATIKA SHERIA MPYA YA MADINI

Waziri wa Nishati na madini Wiliam Ngeleja akiongea na wajumbe wa kamati Bunge ya Nishati na Madini (hawapo pichani)wakati wa mkutano wa siku mbili kujadili maeneo mbalimbali ya mabadiliko katika sheria ya madini ya mwaka 1998 na hatimaye kupata sheria mpya ya madini itakayotoa miongozo ya namna nchi itakavyofaidika kutokana na rasilimali hiyo leo wilayani Bagamoyo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kazi na kamati ya Bunge kujadili maeneo ya mabadiliko katika sheria ya madini ya mwaka 1998 na hatimaye kupata sheria mpya ya madini itakayotoa miongozo ya namna nchi itakavyofaidika kutokana na madini leo wilayani Bagamoyo.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa kazi na kamati ya Bunge kujadili maeneo mbalimbali ya mabadiliko katika sheria ya madini ya mwaka 1998 na hatimaye kupata sheria mpya ya madini leo wilayani Bagamoyo.

Msomaji
Bagamoyo

Thursday, January 14, 2010

Rais Kikwete ahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Guebuza Msumbiji

Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji akinyoosha juu katiba ya Msumbiji muda mfupi baada ya kula kiapo kuendelea kuingoza nchi hiyo kwa muhula wa pili wa Urais katika sherehe zilizofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Maputo.Kushoto ni Rais wa Mahakama ya katiba wa Msumbiji Luis Mondlane aliyemwapisha Rais Guebuza.
Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini akiteta jambo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherere za kuapishwa kwa Rais Armando Emilio Guebuza kendelea kuingoza Msumbiji katika muhula wa pili wa Urais jijini Maputo.Katikati ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini akisisitiza jambo wakati akizungumza na Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Armando Emilio Guebuza wa Msumbiji katika ikulu ya Mjini Maputo muda mfupi baada ya Rais Guebuza kuapishwa kuendelea kuingoza nchi hiyo katika muhula wa pili wa urais.

Msomaji
Msumbiji

RAIS JAKAYA AKUBALI KUONGOZA KAMPENI YA "MARALIA HAIKUBALIKI TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA

Aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Mark Green akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Movenpick wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza"
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa katikati akisikiliza jambo wakati aliyerkuwa Balozi Marekani nchini Mark Green alipokuwa akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza Maralia kwenye Hoteli ya Movenpick leo, kulia ni Peter Peter Chernin (Mwenekiti wa Malaria no More Marekani ) ambaye ameungana na Balozi Mark Green katika kampeni hiyo na kulia ni Naibu waziri wa Afya Aisha Kigoda.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetangaza kuwa leo mheshimiwa Raisi Jakaya M. Kikwete amekubali kuongoza kampeni ya Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza . Leo Wizara imeungana na wasanii mashuhuri wa Tanzania, washirika wa kimataifa na viongozi wa serikali, wafanyabiashara na vitengo vya sanaa kulitangazia Taifa tamasha la zinduka hapo tarehe 13 februari katika viwanja vya leaders club jijini Dar es salaam. Tamasha hili ni kwajili ya kuwahamasisha watanzania katika kupambana na malaria.
Mwaka huu, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufanikisha zoezi la utumiaji wa chandarua ya mbu na kutolewa kwa gharama nafuu kwa raia wake. Katika kuhamasisha juhudi hizi, Raisi kikwete na Malaria haikubaliki inahamasisha kila mtanzania kuwa na jukumu la kujilinda mwenyewe na familia yake katika kuidhibiti malaria.
Tanzania, kama kiongozi wa kupambana na malaria ulimwenguni, inahamasisha sekta zote za kijamii zikiwamo sekta za sanaa, biashara, na michezo kujumuika pamoja kupambana na malaria nchi nzima.
Chini ya uongozi wa Raisi na wizara ya afya na ustawi wa jamii kampeni hii ya uhamasishaji imelenga kila jamii ya kitanzania ili kubadili mtazamo wa watanzania juu gonjwa hili la malaria. Matokeo ya juhudi hizi ni kuongeza ujuzi zaidi wa kujikinga na malaria kama kulala ndani ya chandarua kilichowekwa dawa, tambua na itibu malaria mapema na hakikisha unajali na kuangalia afya ya mama mjamzito.
“Waafrika wengi hudhani malaria haiepukiki, na kwamba hakuna wanachoweza kufanya katika kuzuia gonjwa hili. Tunakwenda kuwahakikishia kuwa sio sahihi. Tunaweza kupunguza vifo vitokanavyo na malaria” alisema Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa “pamoja na mheshimiwa Raisi Jakaya M. Kikwete ninaamini kila Mtanzania atajiunga pamoja kutamka kuwa malaria haikubaliki nchini kwetu 2010.
Katika shughuli za mwaka 2010, Raisi Kikwete ataongoza tamasha la kitaifa liitwalo zinduka litakalowashirikisha wasanii mashuhuri wa Tanzania akiwamo msemaji mkuu wa tamasha hili lady Jay dee, Professor Jay, Tanzania House of Talent (THT na wengine wengi. Kupitia vituo vya luninga na redio ujumbe wa tamasha hili utaweza kuwafikia mamilioni ya watanzani na ujumbe mahususi wa kutambua jukumu lao katika kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Kwa kuongezea wasanii mahiri wa Tanzania wametunga wimbo unaozungumzia athari za ugonjwa wa malaria, wimbo uliowashirikisha wasanii 18, ushirikino mkubwa wa wasanii ambao haujawahi kufanywa hapa Tanzania.Wimbo huo umetambulishwa kwa waandishi wa habari na utaimbwa siku ya tamasha la zinduka
Ulimwengu wa muziki unanafasi kubwa katika kufikisha ujumbe kwa watanzania katika kupambana na malaria na kupata mafanikio makubwa katika kupambana na ugonjwa huu, alisema lady jay dee kama msemaji wa kampeni hii “katika tamasha la zinduka watanzania wote wataweza kupaza sauti zao kwa njia ya wimbo kwa nia moja ya kusitisha malaria nchini.
Katika kuisaidia tanzania kupambana na malaria Malaria Haikubaliki itajumuisha shughuli za ushirikiano za kijamii, PSAs, ujumbe kwa njia ya luninga na radio,mabango,ngazi ya jamii,kiutamaduni, matukio ya kimichezo na maonyesho ya barabarani ili kuhakikisha ujumbe wa malaria haikubaliki unaufikia kila familia nchini Tanzania.
Kampeni hii ya kitaifa itakuwa kwenye engo zote za ngazi ya kijamii na kila nyumba kwa kuhamasisha shughuli za kijamii zitakazotolewa na Population Services International ,Johns Hopkins University na shughuli za district advocacy zitakazoongozwa kwa sauti moja. Kwa wakati huo chama cha msalaba mwekundu Tanzania kitakuwa pamoja na katika kampeni za nchi nzima
SPKutoka kwenye jamii ya imani Malaria Haikubaliki imehusisha baraza la kiristo nchini na baraza la kiislam kuwahusisha viongozi wa kiimani na waumini wao kuweka juhudi katika kupambana na malaria nchi nzima
Barani Africa malaria haiathiri maisha ya watu tu bali jamii nzima, malaria inasababisha mtu mmoja kukosa kazini kwa siku kumi na tano ndani ya mwaka na familia inatumia zaidi asilimia 25 ya kipato cha familia katika kutibu malaria barani Africa.
Malaria ni kikwazo katika maendeleo, inakadiriwa barani Afrika dola bilioni 12 kila mwaka zinapotea na asilimia 40 zinatumika katika masuala ya afya.katika kupambana na ugonjwa huu, Tanzania imeweza kuonyesha jinsi Africa peke yake inavyoweza kujikwamua kutoka kwenye mzigo wa malaria na kuendeleza mikakati yake ndani na nje ya mipaka.
Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza inaongozwa na serikali ya Tanzania na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Washirika wengine katika kampeni hii ya kupinga malaria ni Roll Back Malaria Partnership, Malaria No More, Population Services International, Johns Hopkins University Center for Communication Programs, Tanzanian Red Cross, United Against Malaria, MEDA na World Vision with support from the Global Fund.
Msomaji
Dar es salaam

Rais Kikwete awasili nchini Msumbiji

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtoto Queen Kinguti(9) muda mfupi baada ya kuwasili jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Armando Guebuza kuendelea na muhula wa pili wa urais baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Oktoba Mwaka jana.Queen ambaye wazazi wake ni wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji alikuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kumlaki Rais Kikwete na mkewe Mama Salma jana jioni.
Mtoto Queen Kinguti(kushoto) na Mwenzake Khalid Mgidos(kulia) wakiwakaribisha kwa maua Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Armando Guebuza kuendelea na muhula wa pili wa urais

Msomaji
Msumbiji

Tuesday, January 12, 2010

Maadhimisho ya Miaka 46 ya mapinduzi ya Zanzibar yafana Gombani Pemba

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume akikagua gwaride rasmi la vikosi vya ulinzi katika kilele cha shereh za kutimia miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kiwanja cha Gombani Pemba leo tarehe 12/01/2010.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokea salamu ya Heshma ya vikosi vya Ilinzi na Usalama, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika mapema leo Gombani Pemba.
Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima kwa Viongozi ambao walihudhuria katika sherehe za kutimiza miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar leo katika uwanja wa Gombani huko Pemba.Picha/Clarence Nanyaro….VPO
Wananchi mbalimbali kutoka vyama vya siasa vya CCM na CUF wakipita kwa maandamano katika kuadhimisha sherehe za miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Gombani huko Pemba .Wananchi wengi walijitokeza tofauti na miaka iliyopita kufuatia makubaliano ya amani ya hivi karibuni kati Rais Aman Karume wa CCM na Maali seif Sharif Hamad wa CUF.
Msomaji
Zanzibar

RAIS KARUME AZINDUA REDIO JAMII MICHEWENI PEMBA

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mh. Aman Abeid Karume akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa kituo cha Redio Jamii kilichopo Micheweni kilichojengwa kwa nguza za wananchi na Serikali pamoja na shirika la UNESCO katika kusherekea miaka 46 ya mapinduzi ya Zanzibar
Rais Karume akizungumza na mwakilishi wa UNESCO Bi. Vibele Jensen mara baada ya kuzindua kituo cha Redio Jamii kilichopo Micheweni kisiwani Pemba katika kuadhimisha miaka 46 ya mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika leo kisiwani humo.
Msomaji
Zanzibar

Monday, January 11, 2010

Mfurulizo wa matukio ya sherehe za Maadhimisho ya Mapinduzi ya zanzibar

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akikagua uimara wa vigae vilivyoezeka paa la jengo la Ofisi yake inayojengwa katika eneo la Tunguu huko huo Zanzibar katika maadhimisho ya Miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ofisi hiyo inategemewa kuimarisha shughuli za Muungano pindi itakapokamilika muda mfupi ujao. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mustafa Mohamed Ibrahim na Profesa Lekule wa Chuo cha Ardhi na usanifu wa Majengo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano ,Sayansi na Teknolojia Dk Maua Abeid Daftari akijadiliana jambo na Mama Mwanamwema Shein,Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein,muda Mfupi baada ya Dk Shein kuweke jiwe la Msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari Makangale ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 46 ya mapinduzi ya Zanzibar

Msomaji
Zanzibar

Friday, January 8, 2010

KIKWETE AKUTANA NA MABALOZI IKULU KATIKA SHERRY PART.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. rais J. Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi mbali mbali leo mara baada ya parti aliyowaandalia Ikulu jijini jana.

Friday, January 1, 2010

MAREHEMU MZEE RASHID MFAUME KAWAWA ALIVYOAGWA VIWANJA VYA KARIMJEE JIONI HII

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa marehemeu Mzee Rashid Mfaume Kawawa katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo jioni Marehemu mzee Kawawa anatarajiwa kuzikwa kesho majira ya saa 7:00 mchana nyumbani kwake Kunduchi Madale.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiifariji familia ya Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa muda mfupi baada ya kutoa heshima za mwisho katika ukumbi wa Karimjee, jijinji Dar es Salaam leo Viongozi wa serikali, Vyama, mabalozi na wawakilishi wa mashirika mbalimabli pamoja na Ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika mstari kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Rashid Kawawa.
Rais Jakaya Kikwete katikati akiwa amekaa wakati dua mbalimbali zilipokuwa zikisomwa leo jioni kwenye ukumbi wa Karimjee kabla ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Rashid Mfaume Kawawa kushoto ni Makamu wa Rais Mh. Dr. Ally Mohamed Shein na kulia ni Waziri Mkuu Mh. Pinda na Mwisho kulia ni Mke wa Rais Mama Salama Kikwete wakiwa wamekaa kwa majonzi
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. William Lukuvi akiwatuliza wanafamilia waliokuwa wakilia kwa uchungu mara baada ya Jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Mzee Rashid Kawawa kuwasili katika viwanja vya Karimjee.
Jeneza la Mwili wa Marehemu Mzee Rashid Kawawa likiingizwa kwenye ukumbi wa Karimjee Tayari kwa kutoa heshima za mwisho. Gari Maalum la kijeshi lililobeba mwili wa Marehemu Mzee Rashid Kawawa likiwasili kwenye viwanja vya Karimjee tayari kwa kusomewa Hitma na kutoa heshima za mwisho kabla ya kuzikwa kesho nyumbani kwake Madale Kunduchi.

MZEE RASHID MFAUME KAWAWA AAGA ! KINGUNGE AELEZEA WASIFU WAKE

Tanzania imetangaza maombolezo ya siku saba kufuatia kifo cha mmoja wa waasisi wa chama tawala cha CCM,mzee Rashidi Mfaume Kawawa ambaye alikuwa miongoni mwa waliopigania uhuru wa nchi hiyo Kawawa alikuwa mshirika wa karibu wa baba wa taifa hilo Mwalimu Julius Nyerere na aliwahi kushika wadhifa wa waziri mkuu na makamu wa rais wa Tanzania katika utawala wa Mwalimu Nyerere. Pia aliwahi kuwa katibu mkuu wa CCM kabla ya kustaafu.

Kwa mujibu wa mahojiano ya Sauti ya Amerika mmoja na mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini humo Kingunge Ngombale Mwiru alisema kuwa Mzee Kawawa atakumbukwa kama Simba wa Vita kwa kutetea uhuru wa taifa hilo na pia aliunda shirikisho la Wafanyakazi Tanganyika 1955 ambalo lilishirikiana na TANU katika kutafuta uhuru wa nchi hiyo upande mmoja na kwa upande mwingine haki za wafanyakazi, aliongeza kuwa atakumbukwa kama mchapa kazi na mwaminifu alikuwa waziri mkuu 1962 kwa kuwa Mwl. Nyerere aliamini kuwa ni mtu mwaminifu mchapakakazi na mwenye uwezo wa kuongoza wenzake.

Atakumbukwa kwa kazi ya kujenga taifa jipya akiwa waziri mkuu na baada ya muungano akawa makamu wa pili wa Rais, alishughulikia ulinzi na Vijana na pia kuanzishwa kwa jeshi la wananchi na jeshi la kujenga taifa.

Mwishoni mwa maisha yake alikuwa mshauri mkubwa na mlezi wa Taifa ameonyesha uzalendo na unyeyekevu na hana makuu kazi yake ilikuwa kutumikia watu na ndio maana vijana wa CCM walimteuwa kuwa kamanda wao mlezi wao mkuu.

Alizaliwa Songea mwaka 1926. Alipata elimu ya msingi huko Songea na baadae jijini Dar-es-salaam. Alijiunga na masomo ya sekondari huko Tabora mwaka 1951-1956. Kawawa alikataa nafasi ya kuendelea na masomo ya juu katika chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda ili kuweka bidii zake katika harakati za kugombania uhuru wa Tanganyika.