Balozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Dkt Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kamati ya Maadili na Masuala ya Kimataifa,na familia yake mara baada ya kutunukiwa Tuzo ya the Spirit of the United Nations" 2009" kulia kwa Balozi aliyeshika Tuzo ni Mke wake,Bibi Elizabeth Mahiga.
Dkt Augustine Mahiga Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, amesema Tuzo aliyopewa imemwongezea ari na nguvu ya kujituma zaidi katika kutafuta amani,kutetea utu wa mwanadamu na haki za jamii na katika maeneo ambayo bado mambo hayo yanahitajika. Aliyasema hayo wakati alipokuwa akitoa shukrani zake mara baada ya kutunukiwa tuzo ijulikanayo kama “The Spirit of the United Nations 2009”aliyotunukiwa mapema wiki hii jijini New York.
Umoja wa Mataifa ni daraja linalounganisha tamaduni mbalimbali, rangi na imani katika kujenga utengamano,ushirikiano na maelewano” Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Kamati ya Shirika la Maadili na Masuala ya Kimataifa,hutolewa kwa watu ambao msimamo na utendaji kazi wao katika Umoja wa Mataifa umekuwa ni kielelezo cha misingi na mwelekeo wa Umoja wa Mataifa.Kamati ya Uteuzi ilieleza kuwa Balozi Mahiga amedhihirisha na kujitokeza kama mfano wa mtu anayeamini na kutekeleza misingi hiyo.
Msomaji
New york
No comments:
Post a Comment