Saturday, October 31, 2009

Wanafunzi 592 wameacha shule wilayani Nkasi kwa kipindi cha miaka miwili

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wanafunzi katika moja ya shule alizowahi kuziutembelea.


Wanafunzi 592 wameacha shule wilayani Nkasi kutokana na tatizo la utoro, mimba, kukosa mahitaji na kuugua kwa kipidi cha miaka miwili na hivyo kusababisha kupungua kwa idadi ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya shule ya msingi na sekondari wilayani humo.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa wilaya hiyo Joyce Mgana wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleoa ya wilaya kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyepo ziara ya kikazi ya siku tatu wilayani humo.

Mgana alisema kuwa tangu mwaka 2008 hadi sasa wanafunzi wa shule ya msingi alioacha masomo ni 226 kati ya hao wasichana ni 102 na wavulana 124 na katika shule za sekondari wanafunzi 366 waliacha masomo wakiwemo wasichana 195 na wavulana 171.

"Kuanzia mwaka 2008 hadi sasa wanafunzi 17 wa shule za msingi na wanafunzi 69 kwa upande wa sekondari walipata ujauzito na kesi zao zinaendelea mahakamani, kitendo hiki kinasababisha kwa kiasi kikubwa kushusha maendeleo ya mtoto wa kike",

Mgana alisema.Ili kukabiliana na tatizo la wanafunzi wa kike kupata ujauzito wilaya hiyo iko katika mkakati wa kujenga Hosteli mpya za wasichana zisizopungua tano kwa kila mwaka hadi sasa jumla ya Hosteli saba zinatarajiwa kukamilika kujengwa katika mwaka 2009/ 10.

Mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa, "Kuhusiana na tatizo la utoro mashuleni wanafunzi katika wilaya hii wanakula chakula cha mchana shuleni jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo hili".

Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na ongezeko la watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwani hadi sasa katika shule za msingi kuna watoto yatima 4766 kati yao wasichana ni 2362 na wavulana 2404

Kwa upande wake Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kuhakikisha kuwa watoto wao wanasoma na kufuatilia maendeleo yao mashuleni.

"Ninawasihi kina baba na kina mama msipokee mahari ya watoto wenu msubiri hadi matokeo ya mtihani yametoka kama mtoto amefeli na mzazi anao uwezo wa kumsomesha katika shule ya kulipia ni bora ukampeleka mwanao shuleni kuliko kumuoza jambo ambalo litarudisha nyuma maendeleo yake ", alisema Mama Kikwete.

Aliendelea kusema kuwa Serikali ina makusudi ya kuanzisha shule za Sekondari za kata na kuongeza idadi ya shule za Msingi ili watoto wetu wasome na kupata wataalamu wengi ambao watasaidia kupunguza tatizo la wataalamu tulilonalo hivi sasa.

Wilaya hiyo ina shule za msingi 97 na shule za sekondari za Serikali 18 zilizojengwa kwa kushirikiana na wananchi, jumla ya wanafunzi katika shule za sekondari ni 6066 wasichana 2053 na wavulana 4013 na katika shule za msingi ni 49,428 kati ya hao wavulana ni 24,682 na wasichana ni 24,746.

Taasisi ya WAMA ilivichangia vikundi vya wanawake wajasiriamali vilivyopo wilayani humo Tshs. 1,500,000/= na Umoja wa Wanawake (UWT) Tshs. 500,000 fedha ambazo zitatumika kuinua mitaji ya vikundi hivyo.

Msomaji
Nkasi

Friday, October 30, 2009

Rais Kikwete alivyoweka jiwe la msingi kituo cha Watoto yatima Rungwe

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Lucy Hope Centre Bi.Lucy Mwandosya pamoja na Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya muda mfupi baada ya kuwahutubia wananchi wa Lufilyo,Rungwe wakati wa uwekaji jiwe la Msingi katika jingo la taasisi hiyo uliofanyika jana.Taasisi ya lucy Hope inawahudumia watoto Yatima.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lucy Hope Centre Bi.Lucy Mwandosya na Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya wakishangalia wakati wa hafla ya kuweka jiwe la Msingi katika jingo la taasisi hiyo iliyofanyika huko Lufilyo,Rungwe, mkoani Mbeya jana jioni.Taasisi ya Lucy Hope inawahudumia watoto Yatima kwa kuwalea na kuwapa elikmu katika ngazi mbalimbali
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lucy Hope Centre Bi. Lucy Mwandosya na Mumewe Profesa Mark Mwandosya wakimkabidhi picha iliyochorwa na Bi.Lucy mwandosya inayoonesha ngoma ya utamaduni ya Rungwe wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi katika jengo la taasisi hiyo huko Lufilyo Rungwe jana jioni.

Msomaji
Mbeya

Thursday, October 29, 2009

Balozi Mahiga Alivyopokea Tunzo ya Spirit of the United Nations 2009!!

Balozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Dkt Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Kamati ya Maadili na Masuala ya Kimataifa,na familia yake mara baada ya kutunukiwa Tuzo ya the Spirit of the United Nations" 2009" kulia kwa Balozi aliyeshika Tuzo ni Mke wake,Bibi Elizabeth Mahiga.
Dkt Augustine Mahiga Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, amesema Tuzo aliyopewa imemwongezea ari na nguvu ya kujituma zaidi katika kutafuta amani,kutetea utu wa mwanadamu na haki za jamii na katika maeneo ambayo bado mambo hayo yanahitajika. Aliyasema hayo wakati alipokuwa akitoa shukrani zake mara baada ya kutunukiwa tuzo ijulikanayo kama “The Spirit of the United Nations 2009”aliyotunukiwa mapema wiki hii jijini New York.
Umoja wa Mataifa ni daraja linalounganisha tamaduni mbalimbali, rangi na imani katika kujenga utengamano,ushirikiano na maelewano” Tuzo hiyo ambayo hutolewa kila mwaka na Kamati ya Shirika la Maadili na Masuala ya Kimataifa,hutolewa kwa watu ambao msimamo na utendaji kazi wao katika Umoja wa Mataifa umekuwa ni kielelezo cha misingi na mwelekeo wa Umoja wa Mataifa.Kamati ya Uteuzi ilieleza kuwa Balozi Mahiga amedhihirisha na kujitokeza kama mfano wa mtu anayeamini na kutekeleza misingi hiyo.
Msomaji
New york

Thursday, October 22, 2009

Makala: Siasa za Ushindani na Mustakabali wa Taifa

Na Mhe. Pius Msekwa,

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)

Malengo na Changamoto za siasa za Ushindani.
1. Malengo

1.1 Baada ya mchakato mrefu wa maandalizi yake, hatimaye tarehe 1 Julai, 1992, Tanzania ilirejea katika mfumo wa siasa za ushindani baina ya vyama mbalimbali vya siasa.

Hatua ya kwanza ya mchakato huo ilichukuliwa mwezi Februari 1991, ambapo Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi, katika mkutano wake wa Februari, 1991, “baada ya kutafakari kwa makini suala la mageuzi yaliyokuwa yanatokea katika Afrika na duniani kote kwa jumla, iliamua uanzishwe mjadala wa kitaifa juu ya suala la ama kuendelea na mfumo wa chama kimoja cha siasa, au kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini Tanzania”.

Katika kutekeleza uamuzi huo, mnamo mwezi Machi, 1991, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitangaza kuundwa kwa Tume ya kuratibu mjadala wa kitaifa juu ya hoja hiyo (Tume ya Nyalali); na baada ya hapo kuishauri serikali kama ambavyo Tume hiyo itaona kuwa inafaa.

Tarehe 11 Desemba mwaka huo huo, Tume hiyo iliwasilisha kwa Rais taarifa yake ya awali, ikipendekeza mabadiliko yafanyike ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi vya siasa. Tarehe 16 Januari, 1992, Tume iliwasilisha kwa Rais taarifa yake ya mwisho yenye mapendekezo kamili kuhusu hadidu zote za rejea ambazo Tume hiyo ilikuwa imepewa.

Rais naye aliwasilisha mapendekezo hayo ya Tume kwenye vikao husika vya Chama Cha Mapinduzi. Hatimaye Mkutano Mkuu maalum wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika mjini Dar es Salaam tarehe 18 hadi 19 Februari, 1992, ulipitisha azimio la kukubali kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.

1.2 Changamoto kubwa wakati huo ilikuwa ni suala la ufinyu wa demokrasia. ‘Mageuzi’ ambayo Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM “iliyatafakari kwa makini” katika mkutano wake wa Februari 1991, yalikuwa ni mageuzi ya kutoka mfumo wa chama kimoja cha siasa, ambao ulikuwa umetawala katika nchi nyingi za Afrika na Ulaya ya Mashariki wakati huo, na kuingia katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Mageuzi hayo katika nchi za Afrika yalichochewa na wimbi kubwa la mageuzi ya kisasa lililozikumba nchi za Ulaya Mashariki katika kipindi hicho, ambazo zilikuwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha kikomunisti, ambayo yalifikia kilele chake mwaka 1989.

Lakini pamoja na kuchochewa hivyo na mageuzi yaliyotokea katika nchi za Ulaya Mashariki, zilikuwapo vile vile sababu nyingine za ndani ya nchi hizi, ambazo pia zilichangia kuibuka kwa madai ya kutaka kufanyika kwa mageuzi ya mfumo wa kisiasa.

Kwa upande wa Tanzania, sababu hizo ni pamoja na matatizo makubwa ya kiuchumi, ambayo watu wengi walihisi kuwa yalisababishwa na ukiritimba wa mfumo uliokuwapo wa chama kimoja cha siasa na sera zake za ukiritimba katika uchumi.

2. Changamoto
Changamoto za woga wa kuingia katika siasa za ushindani:
Changamoto kubwa iliyojitokeza katika mjadala wa mabadiliko hayo, ilikuwa ni hofu, au woga, kuhusu mabadiliko yenyewe. Katika taarifa yake kwa Rais, Tume ya Nyalali ilieleza kwamba “wengi waliopendelea kuendelea na mfumo wa sasa wa chama kimoja, walikuwa na woga wa kuchagua kitu wasichokijua” (fear of the unknown). Tume hiyo ilihisi kwamba hiyo ndiyo sababu kubwa iliyosababisha asilimia themanini (80%) ya wananchi wote waliohojiwa na Tume hiyo wachague kuendelea na mfumo wa chama kimoja cha siasa. Lakini kwa busara zake, bado Tume hiyo ikapendekeza kwamba yafanyike mabadiliko ya mfumo huo. Na Chama cha Mapinduzi, kwa busara zake, kikakubali pendekezo hilo.

Hata hivyo, woga huo haukuwa kwa wananchi peke yao, kwani hata baadhi ya Hadidu za Rejea zenyewe zilionyesha dalili za wasiwasi, endapo Tume itapendekeza yafanyike mabadiliko ya mfumo wa siasa. Kwa mfano, Tume ilielekezwa:

(i) “Kutoa ushauri na mapendekezo juu ya haja, hekima, na matokeo ya kuendelea na chama kimoja cha siasa, au kubadili mfumo huo kwa kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa bila kuathiri malengo muhimu na misingi ya mwelekeo wa shughuli za serikali, pamoja na haki na wajibu muhimu katika jamii”.

(ii) Kuzingatia, kuchambua, na kufafanua athari au manufaa ya mabadiliko yoyote yale katika mfumo uliopo, hasa kuhusu Muungano wetu, umoja wa Watanzania, amani ya nchi na maelewano yaliyopo miongoni mwa Watanzania wote bila kujali kabila, dini, rangi au jinsia yao.

(iii) “Kupendekeza njia za Kikatiba, kisheria na kisiasa za kujikinga na athari zozote za kisiasa au za kiusalama za kubadili au kutobadili mfumo wetu wa siasa, kwa shabaha ya kulinda umoja wa Taifa letu, Muungano wa nchi yetu na maelewano ya Watanzania wote bila kujali kabila, dini rangi au jinsia yao”.

(iv) “Kuzingatia na kufafanua athari za mabadiliko yoyote, endapo yatapendekezwa na Tume, katika suala zima la nafasi ya Zanzibar katika Muungano; na pia kuangalia kwa undani kama itakuwa ni kwa faida (salama) ya Zanzibar kutekeleza mabadiliko ya mfumo uliopo wa kisiasa, kwa kuzingatia historia ya kisiasa ya Zanzibar pamoja na tabia ya watu wa Zanzibar”.

Ukiyaangalia kwa undani zaidi, maelekezo hayo yanaashiria kuwapo kwa wasiwasi juu ya kubadilisha mfumo uliokuwapo, kwani yanasisitiza “kuchambua na kufafanua athari za mabadiliko hayo” na “kupendekeza njia za kikatiba. Kisheria na kisiasa, za kujikinga na athari za kisiasa au kiusalama za kubadili mfumo wetu”.

Lakini hofu kubwa zaidi ilikuwa ni kwa upande wa Zanzibar. Ndiyo sababu Tume ilielekezwa “kuangalia kwa undani kama itakuwa ni kwa faida (salama) ya Zanzibar kutekeleza mabadiliko ya mfumo uliopo, kwa kuzingatia historia ya kisiasa ya Zanzibar na tabia ya watu wa Zanzibar”. Maelekezo hayo yanaashiria kushinikiza kwamba Zanzibar isihusishwe katika mabadiliko ya mfumo wa kisiasa, kutokana na hofu hizo zilizotajwa.

Tume ya Nyalali inastahili kupongezwa kwa kazi yake nzuri iliyowezesha mabadiliko ya mfumo kufanyika kiulaini, kutokana na mapendekezo yake mazuri ya hatua za kuchukuliwa ili kujikinga na athari zile zilizokuwa zimehofiwa kuwa zingetokea. Tume ya Nyalali ilipendekeza kama ifuatavyo:

(1) Ili kulinda na kuhifadhi demokrasia, umoja, hali ya amani, utulivu wa kisiasa na mshikamano wa Taifa letu zitungwe sheria zitakazohakikisha kwamba:-

(a) Uandikishwaji wa vyama vya siasa nchini uwe ni jambo la Muungano.

(b) Vyama vya siasa viwekewe masharti maalum ambayo yatazingatia maslahi ya Taifa, hususan:

· Viwe ni vyama vya kitaifa (kwa maana ya pande zote mbili za Muungano); na visiwe vyama vyenye mwelekeo wa kugawa nchi au wananchi kwa msingi wa ukabila, dini, kanda, jinsia, rangi, au upande mmoja wa Muungano.

· Viwe ni vyama vinavyoanzishwa na wananchi wenyewe wenye nia ya kushirikiana katika kulinda matunda ya uhuru, na kuleta maendeleo zaidi ya nchi yetu.

· Viwe ni vyama vyenye lengo la kuendeleza na kuimarisha Muungano wetu. Visiwe vyama vyenye nia ya kuvuruga au kuvunja Muungano huu.

· Viwe ni vyama vinavyokubali misingi ya usawa wa haki na heshima kwa raia wote wa Tanzania.

· Viwe ni vyama vinavyokubali kueneza siasa na sera zake kwa misingi ya hoja. Yaani visiwe vyama vinavyotumia uchochezi, fujo, au mabavu katika kufikia malengo yake.

Mapendekezo hayo yote yalikubaliwa na kuingizwa katika Katiba ya nchi, na vile vile katika Sheria ya Vyama vya Siasa, na. 5 ya 1992. Sheria hiyo pia ilitoa tafsiri sahihi ya chama cha siasa, kwamba;

“Political Party” means any organized group formed for the purpose of forming a government or a Local Government Authority within the United Republic through elections; and for putting up or supporting candidates for such elections”.

3. Changamoto baada ya kuingia katika siasa za ushindani:

Changamoto nyingine zaidi zimejitokeza katika uendeshaji wa mfumo huu wa siasa za ushindani. Miongoni mwake ni hizi zifuatazo:-

(1) Hali ya kuwa na ‘vyama vingi lakini sera moja’. Hii imekuwa ni changamoto kwa sababu nadharia ya ubora wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa inaeleza kwamba inawapatia wananchi ambao ni wapiga kura, fursa ya kuchagua chama chenye sera ambazo zinawavutia zaidi, na wangependa kukiweka chama chenye sera hizo madarakani ili kiweze kuzitekeleza. Lakini katika nchi maskini kama Tanzania, sera pekee itakayowanufaisha wananchi wote, ni sera ya kuwaondoa katika dimbwi hilo la umaskini kwa kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hakuna chama kinachoweza kuwa na sera ambayo ni tofauti na hiyo.

Matokeo yake ndiyo hayo ya ‘vyama vingi, sera moja’. Kwa hiyo wananchi wanakosa fursa ya kuchagua sera iliyo bora zaidi miongoni mwa sera za vyama mbalimbali vilivyopo. Kutokana na hali hiyo, uchaguzi unakuwa ni zoezi tofauti na lile linaloelezwa katika nadharia ya demokrasia ya vyama vingi.

(2) Hali ya kutokuwa na chama ambacho kinaweza wakati wowote kuunda ‘serikali mbadala’, kutokana na nguvu yake ilivyo ndani ya Bunge, kwa maana ya wingi wa Wabunge wake.

Nadharia nyingine ya ubora wa demokrasia ya vyama vingi inasema kwamba wakati wote unakuwapo uwezekano wa kuunda serikali mbadala, endapo serikali iliyopo madarakani itakuwa imeondolewa madarakani kwa kura za Wabunge walio wengi. (vote of no confidence).

Tukio la aina hiyo liliwahi kutokea Uingereza mwaka 1979, wakati serikali iliyokuwa imeundwa na chama cha Labour Party ilipoondolewa kwa kura za Wabunge 311 waliosema ‘ndiyo’ kwa hoja ya kuiondoa serikali hiyo madarakani; dhidi ya kura 310 za Wabunge waliosema ‘hapana’. Hivi karibuni, Serikali ya India pia ilipata mtihani kama huo, lakini iliweza kupata kura za ushindi na kubaki madarakani.

Hapa kwetu, matokeo ya kura katika awamu tatu za uchaguzi mkuu tangu tulipoingia katika mfumo wa siasa za ushindani, yanaonyesha kwamba nguvu ya upinzani Bungeni imekuwa ikizidi kupungua katika kila uchaguzi mkuu. Nguvu ya vyama vya upinzani vyote kwa pamoja ndani ya Bunge baada ya uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995, ilikuwa ni chini kidogo ya 20% ya viti vyote vya majimbo Bungeni, kwani CCM ilipata 80.17% ya viti hivyo.

Katika uchaguzi mkuu uliofuatia wa mwaka 2000, CCM ilipata 87.5% ya viti vyote vya majimbo Bungeni; na katika uchaguzi mkuu wa tatu wa mwaka 2005, CCM ilipata 88.8% ya viti vyote vya majimbo Bungeni.

Hali hiyo inaashiria mambo mawili, kwamba:-

(a) Serikali ya CCM haiwezi kuondolewa madarakani kwa kura za Wabunge walio wengi (majority) wanaotaka kuiondoa madarakani, kwa sababu hawapo; na

(b) Hata kama vikiamua kushirikiana, vyama vya upinzani bado havina idadi ya Wabunge wa kutosha kuviwezesha kuunda serikali mbadala.

Hata hivyo, suala la ushirika siyo rahisi katika jambo hili. Wakati fulani baadhi ya vyama vya siasa vya India vilijaribu kuungana ili kuunda serikali, baada ya kukosekana chama chochote ambacho kilipata idadi ya kutosha ya wabunge kukiwezesha kuunda serikali peke yake. Vyama vilivyokubaliana kuungana bado havikuwa na idadi ya kutosha ya Wabunge, kwa hiyo wakajaribu kuunda ‘serikali ya wachache’ (minority government). Serikali hiyo ilikaa madarakani kwa muda wa siku 13 tu kabla Bunge jipya halijakutana. Katika muda huo, walijaribu kupata washirika wengine, lakini wakashindwa. Mwandishi mmoja wa mambo ya kisiasa huko India aliukejeli muungano wao huo kwa kusema:

“It was like a cemetery. Those who were inside could not come out, and those who were outside had no wish to go in”.

4. Changamoto ya mfumo wa uchaguzi:

Kwa upande wa uchaguzi, Tanzania inaendelea kutumia mfumo wa uchaguzi tuliorithishwa na Waingereza, ambapo kila chama cha siasa kinasimamisha wagombea wake katika kila jimbo la uchaguzi, endapo kina uwezo wa kufanya hivyo.

Mfumo huo una matatizo mawili. Kwanza, ni kwamba katika macho ya wapiga kura wengi, mfumo huo haushindanishi vyama vya siasa, bali unashindanisha watu wanaogombea uchaguzi huo. Ndiyo sababu katika baadhi ya majimbo, imewahi kutokea kwamba mgombea aliyejaribu kusimama kwa tiketi ya CCM lakini akokosa uteuzi wa chama hicho, anashauriwa na wapiga kura ahamie chama kingine chochote ili waweze kumchagua. Na kweli anachaguliwa kwa tiketi ya chama hicho alichohamia. Hii inamaanisha kwamba wapiga kura hao wanamtaka huyo mtu, na siyo chama chake! Ndiyo sababu wanamshauri ahamie chama kingine chochote, bila kujali ni chama gani.

Pili, ni kwamba kwa sababu hiyo ya kushindanisha watu badala ya kushindanisha vyama, mfumo huo unatoa mwanya kwa wenye uwezo mkubwa wa fedha, kutumia fedha zao kujinunulia ushindi. Kwa maneno mengine, mfumo huo unatoa mwanya kwa rushwa kutumika katika uchaguzi.

Tatu, uzoefu wa awamu tatu za uchaguzi mkuu zilizopita, unaonyesha kwamba baadhi ya vyama vinashindwa kusimamisha wagombea katika majimbo yote 232 yaliyopo, zaidi kwa sababu ya gharama zake kuwa kubwa, miongoni mwa sababu nyingine.

Kwa ajili hiyo, tayari yapo mawazo miongoni mwa wananchi, kwamba pengine ingefaa tufikirie uwezekano wa kutumia mfumo wa uwakilishi Bungeni unaotokana na uwiano wa kura za kila chama cha siasa (proportional representation). Katika kanda ya SADC, mfumo huo ndio unaotumika Msumbiji, Afrika Kusini na Namibia, miongoni mwa nchi nyingi nyingine, hasa za Ulaya. Ni mawazo ambayo yanastahili kufanyiwa kazi kwa kupima na kulinganisha uzuri na ubaya wake, ili ukionekana kuwa unafaa, uweze kutumika pia katika nchi yetu.

5. Changamoto ya siasa za ushindani Zanzibar:

Tumekwisha kutaja mapema katika makala haya, ile hofu iliyoelezwa katika hadidu za rejea za Tume ya Nyalali, kwa kuitaka Tume hiyo “kuzingatia kwa undani kama itakuwa ni kwa faida (salama) ya Zanzibar kutekeleza mabadiliko ya mfumo wa kisiasa uliopo, kwa kuzingatia historia ya kisiasa ya Zanzibar, na tabia za watu wa Zanzibar”.

Ni kweli kwamba utekelezaji wa siasa za ushindani baina ya vyama vya siasa umeleta mgogoro katika utawala wa Zanzibar, ambapo kila uchaguzi mkuu umefuatiwa na vitendo vya ghasia kutokana na chama cha CUF kutokutambua matokeo ya uchaguzi huo. Mazungumzo ambayo yamekuwa yakifanyika baina ya vyama vya CCM na CUF yaliwezesha kupatikana kwa MUAFAKA I na II; lakini matatizo ya kisiasa bado yanaendelea. Kwa hiyo juhudi za kutafuta MUAFAKA III vile vile zinaendelea.

6. Mwisho

Katika kuhitimisha makala haya, ni vema kutambua na kupongeza kuwapo kwa chombo rasmi cha mazungumzo kinachowaweka pamoja Wakuu (Wenyeviti na Makatibu Wakuu) wa vyama vyote vyenye Wabunge. Chombo hicho kinaitwa Tanzania Center for Democracy (TCD), na kinashirikisha pia Wakuu wa vyama vingine vyenye usajili wa kudumu, ambavyo kwa wakati uliopo havina wabunge. Kuwapo kwa chombo hiki ni hatua muhimu sana ya kujenga maelewano na ushirikiano baina ya vyama baada ya kumalizika kwa uchaguzi.

Mantiki yake ni kwamba wakati wa uchaguzi ni wakati wa ushindani mkali, kwa kila chama kuwania kupata kura nyingi iwezekanavyo. Lakini baada ya uchaguzi mkuu kumalizika, ni jambo zuri sana kwamba tumeweza kuwa na chombo kama hicho cha ushirikiano baina ya vyama vya nje ya Bunge. Na kama ambavyo vyama vyenyewe vyenye Wabunge vinapata ruzuku kutoka serikalini, chombo hiki pia kinapata ruzuku kutoka serikalini kusaidia uendeshaji wa shughuli zake.


Mungu ibariki Tanzania

Wednesday, October 21, 2009

TAHARIFA YA MSIBA

MAMA MZAZI WA MWENYEKITI WA CCM TAWI LA MAREKANI AFARIKI DUNIA
MWENYEKITI WA CCM TAWI LA MAREKANI, MH. MICHAEL NDEJEMBI ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MAMA YAKE MZAZI BI. ELIZABETH BENJAMINI NDEJEMBI, KILICHOTOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO TAREHE 21/10/2009 HUKO DODOMA, TANZANIA.
SHUGHULI ZOTE ZA MAANDALIZI YA MSIBA ZINAENDELE NA TUTAENDELE KUWAPATIA TAHARIFA ZAIDI KUHUSIANA NA MSIBA HUU
KWA SALAAM ZA RAMBIRAMBI NA KUTOA POLE KWA NDUGU YETU MICHAEL NA FAMILIA, UNAWEZA KUFIFA NYUMBANI KWAKE AU KWA NJIA YA SIMU
ADRESS KAMILI YA NYUMBANI KWA BWANA MICHAEL NI:
2602 WEASTERLAND DRIVE A8
HOUSTON, TEXAS 77063
SIMU NI:
713-384-4567
U.S.A
MUNGU AIPUMZISHE KWA AMANI
ROHO YA MAREHEMU PEPONI
-AMEN

Sunday, October 11, 2009

WHY INVEST IN TANZANIA

1-IVESTMENT INCENTIVES AND GUARANTEES
Tanzania offers a well-balanced and competitive package of fiscal incentives in comparison with other African countries. Aiming at providing competitive fiscal regime on foreign trade, Tanzania has signed double taxation treaties with Denmark, India, Italy, Norway, Sweden, Kenya, Uganda, Zambia and Finland. Countries with which negotiations are continuing include South Africa, Republic of Korea, Zimbabwe, United Arab Emirates, Russia, Seychelles, Mauritius, Egypt, Yugoslavia and Oman.Investments in Tanzania are guaranteed against nationalisation and expropriation. Tanzania is a signatory of several multilateral and bilateral agreements on protection and promotion of foreign investment. Among other international agreements and membership, Tanzania is a member of Multilateral Investment Guarantee Agency (MIGA) and International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID).

2-ABUDANT NATURAL RESOURCES
Tanzania’s untapped natural resources offer a wide range of investment opportunities; arable land, minerals and natural tourist attractions are all awaiting potential investors. Tanzania is internationally renowned for its abundance of wildlife attractions and unexploited mineral reserves. These sectors (Mining and Tourism) are the leading recipient of foreign investment flow and are tipped to become the “growth sectors” of the economy.

3-STABLE INVESTMENT POLICY AND “ONE STOP FACILITATIVE CENTRE”
Tanzania Investment Centre (TIC)The pro investment attitude by Government is clearly demonstrated by the innovative investment legislation, the increasing number of foreign direct investments in the country and economic and structural reforms that have led to substantial progress in establishing a functioning market economy. Institutional support for priority investment projects is readily available from the Tanzania Investment Centre (TIC) and other Government institutions.TIC is the focal point for investors. It is a first point of call for potential investors. It is an efficient and effective investment promotion agency, a “one stop facilitative centre for all investors”, engaging in the business of marketing Tanzania as an investment destination. In order to strengthen and expedite facilitation services, 7 senior officers from Government or its executive agencies have been permanently stationed at TIC to serve investors under the general direction of the TIC Executive Director. Presently these officers include those from:Lands DepartmentTanzania Revenue Authority (TRA)Immigration DepartmentLabour DivisionDirectorate of Trade

4-BUSINESS REGISTRATION & LICENSING AGENCY(BRELA)
In response to Scholars and consultants recommendation, TIC is currently undertake targeted promotion of investments internally and abroad based on thorough research. Market research-driven investment promotion tends to be more efficient in cutting costs of promotion and achieving more desirable investment outcome

5-STABLE MACROECONOMIC PERFORMANCE AND FISCAL REGIME
Tanzania had been carrying out successful economic and structural reforms, which have improved economic performance and sustained growth. These achievements are based on solid foundations of political and economic reform undertaken by the Government since 1986, placing Tanzania in a position where a prolonged period of high GDP growth rates is expected. In addition, Tanzania has a stable fiscal regime with sustainable level of inflation. Under its economic recovery program, Tanzania increased revenue streams and substantially reduced spending. Continuous decline in the rate of inflation is mainly the result of prudent fiscal and monetary policies. However, Tanzania has to reduce further the cost of doing business to stimulate supply response at micro-level. This is important in order to complement the current achievements on macroeconomic and political stability by greater efforts to improve the investment climate.

6-PRIVATE SECTOR DEVELOPMENT DURING THE PAST DECADE
Tanzania has distinguished itself as one of the few African countries that have radically transformed their economies. Successes of these reforms are reflected in the country’s strong macroeconomic fundamentals with consistently increasing growth rates, consistent falling inflation and increasing inflow of FDI. One of the factors that contributed to this success is the country’s unwavering commitment to build a strong private sector. This achievement is a result of a number of measures to reform the business environment by improving transparency of the investment process and encouraging stakeholder participation. A number of institutions and forums have been put in place to ensure a broader participation of different stakeholders including representatives of the private sector, trade unions, professional associations, media, and Government departments and other representatives of civil society. Existing institutions with stakeholder participation in the investment process include: Tanzania National Business Council; Investor’s Roundtables; Special Reform Task Forces; Investment Seminars; Board membership in TIC and other Government Agencies.The Tanzania National Business Council 50% government and 50% Private Sector is the lead dialogue institution where government interact with diverse stakeholder representatives from the private sector for dialogue on strategic issues related to the investment process and business environment in Tanzania. The Council is chaired by the President of Tanzania. The President’s commitment to transparency manifests itself in the workings of the roundtables such as the local Investor’s Round Table (LIRT), International Investor’s Roundtable (IIRT) and the Chief Executive Officers (CEO) Roundtable where the President meets private sector representatives on a regular basis to discuss specific issues aimed at improving Tanzania’s business competitiveness.

7-INFRASTRACTURE FACILITIES
Infrastructure is one of the key investment drivers of which Tanzania is struggling to improve. There is a sustained programme for building good quality roads. Two railway networks connect 14 out of 20 cities and the neighbouring country of Zambia. There are also international and domestic airports linking Tanzania to the world. The three major ports of Dar es Salaam, Tanga and Mtwara function as hubs for traffic emanating from, and destined to land locked neighbouring countries of Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia, Malawi, and Democratic Republic of Congo.However, Tanzania has to make further improvement in the investment climate, especially in the provision of infrastructure including competitive public utilities and taxation area (multiplicity of taxes especially at local government level) and.

8-PEACE AND STABILITY
Tanzania is free of ideological confrontations, ethnic problems and labour disputes. It is a centre of economic and political stability in Sub Saharan Africa. Multi party democracy adopted in 1992 has not disturbed the peaceful political climate of the country. The political scene is characterised by parliamentary democracy and public consensus on key social and economic priorities.

9-LABOUR SKILLS AND AVAILABILITY
Access to skilled labour is a key priority for companies competing in African economies. The Government has made a long-term commitment to develop a pool of well-trained and educated specialists. The Government has increased its education budget significantly compared to the previous budget. Thus Tanzania has to further improve human capabilities and encourage technology transfer as a precondition for enhancing productivity of investment and attaining the
desired level of competitiveness

Ndejembi michael.

Tuesday, October 6, 2009

CCM NCHINI MAREKANI WAKUTANA NA MH. BENARD MEMBE

Uongozi wa Chama cha Mapinduzi - Marekani wiki iliyopita ulikutana na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa ambae pia ni waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mh. Benard Membe mjini Houston Texas.
Waziri Membe akiwa katika mazungumzo na viongozi wa CCM Marekani katika Hotel ya Reinnesance Jijini Houston Ijumaa tar. 2 Oktoba 2009.
Viongozi wa CCM Marekani walipokutana na Mh. waziri Membe, kutoka kushoto ni Deogratius Rutabana ambae ni mwenyekiti wa CCM Marekani Shina la Missouri, Ndugu Juma Maswanya mlezi wa tawi, Mh. Sefue balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mh. Membe, Ndugu Michael Ndejembi mwenyekiti wa tawi, bi. Zainab Janguo katibu siasa na uenezi wa tawi, bi. Beatrice Mlengule mmoja wa wanachama.
Bi. Radhia Naima Msuya balozi idara ya Marekani na bara la Ulaya akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM Marekani Jijini Houston.

YANGA WAIBWAGA SIMBA 3 - 2.

Mh balozi Sefue akihutubia umati uliojitokeza kwenye ukumbi wa safari kuipongeza timu ya Yanga baada ya kuibuka kidedea kwenye pambano la watani wa jadi lililofonyika katika viwanja vya Memorial Park jijini Houston.
kepteni wa timu ya yanga ndugu Charles Ngalawa (mwenye T-shirt jeupe) pamoja na moja wa wachezaji(ndg Andrew Sanga) akiwa amenyanyua juu kombe la ushindi mara baada kukabidhiwa na Mh. balozi,Kulia mwa balozi ni Dr. Tenende.
Rais wa jumuia ya Watanzania waishio majimbo ya Kansas city Missouri na Kansas ndugu Deogratius Rutabana (wa kwanza kushoto) akiwa na mwenyekiti wa CCM Marekani ndugu Michael Ndejembi (katikati) na Rais mstaafu wa jumuia ya watanzania waishio jijini Houston ndugu David Mrema.
Mweka hazina wa CCM Marekani ndugu Innocent Batamula (wa kwanza kulia) katika picha ya pamoja na wana-Houston, kutoka kulia ni Dr. Tenende, Juma maswanya na Michael.
Rais wa sasa wa jumuia ya watanzania waishio Houston ndugu Simon Makangula (mwenye T-shirt) akiwa na baadhi ya wana jumuia ndugu Kim (mwenye shati jeusi) na ndugu Mathew(aliyeshika kombe).
Wasanii Seki na Lambert wakitoa burudani maridhawa kwenye ukumbi wa Safari Jijini Houston. Wasanii hao walizikonga vilivyo nyoyo za mamia ya washabiki waliohudhuria sherehe za kuwakabidhi kombe kwa timu ya Yanga -Houston inayoundwa na mashabiki ya Yanga.

Monday, October 5, 2009

Rais Kikwete alipojiandikisha kwa ajili ya Uchaguzi wa Viongozi ngazi za Mitaa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwaajili ya uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya mtaa katika kituo cha Shule ya Msingi Bunge,kilichopo jijini Dar es Salaam jana mchana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na karani wa kituo cha Shule ya msingi Bunge muda mfupi baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi wa Viongozi ngazi ya mitaa.

Msomaji
Dar es salaam

Thursday, October 1, 2009

SERA YA MAJI YAJADILIWA NA WADAU WA MAJI NA TAASISI ZAKE

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Marck Mwandosya akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kufungua warsha ya Mkakati wa pamoja wa kuangalia upya sera ya maji iliyoanza leo katika jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es alaam, Warsha hiyo inashirikisha wadau mbalimbali wa maji na Taasisi zake na itaendelea mpaka kesho.
Washiriki mbalimbali wa warsha ya Mkakati wa pamoja wa kuangalia upya sera ya maji inayofanyika leo Ubungo Plaza jijini Dar es salaam wakisikiliza kwa makini wakati Waziri wa maji na umwagilaji Prof Marck Mwandosya alipokuwa akifungua warsha hiyo.
Msomaji
Dar es salaam