Monday, March 29, 2010

Rais Kikwete apokea vifaa mbalimbali kutoka China

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng mara baada ya kuwasili Ikulu leo jijini Dar es salaam kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vikiweo vifaa vya usafiri, vifaa vya nyumbani na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 51.
Rais Jakaya Kikwete akiagalia msaada wa baiskeli zilizotolewa na nchi ya China ikiwa ni sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 51 vilivyotolewa na nchi hiyo leo Ikulu jijini Dar es salaam.Kulia kwake ni Balozi wa China Liu Xinsheng aliyekabidhi msaada huo.
Rais Jakaya Kikwete akikagua pikipiki ikiwa ni sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na nchi ya China kupitia kwa Balozi wa nchi hiyo Liu Xinsheng (kulia) kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo nchini. Makabidhiano hayo ya vitu mbalimbali vikiweo vifaa vya usafiri, vifaa vya nyumbani na michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 51 yamefanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam
Msomaji
Dar es salaam

Sunday, March 28, 2010

Rais Kikwete aongoza kikao cha Kamati kuu jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akingoza kikao cha Kamati kuu ya CCM ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Wengine katika picha ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Amani Abeid Karume, Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba, Makamu wa CCM Bara Pius Msekwa, Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi,Rais mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Mkapa na Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha.
Badhi ya wajumbe wa kamati kuu ya CCM wakiwa katika kikao ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi Chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Msomaji
Dar es salaam

Ufunguzi rasmi wa mkutano wa 122 wa umoja wa Mabunge Duniani, Bangkok

Spika wa Bunge, Mhe. Samuel Sitta akichangia katika mjadala kuhusu maswala ya kisiasa na kiuchumi Duniani wakati wa Mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika mjini Bangkok, Thailand, wikiendi hii.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 122 wa IPU katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa rasmi jana.

Spika wa Bunge, Mhe. Samuel Sitta, akifuatilia kwa makini ufunguzi rasmi wa mkutano wa 122 wa umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ulioanza rasmi jana mjini Bangkok, Thailand kwa kufunguliwa na Mtoto wa Mfalme wa nchi hiyo, Princess Maha Chakri Sirindhorn . Walioketi kusho ni balozi wa Tanzania nchini Malaysia anayesimamia pia Thailand, Mhe. Cisco Mtiro, Mhe, Dkt Christine Ishengoma, Mhe. Idris Mtulia na Mhe. Suzan Lyimo.
Binti Mfalme wa Thailand, Malkia Maha Chakri Sirindhorn, akifungua rasmi mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika ukumbi wa Centara Bangkok Convention Centre. Mkutano wa huo umeanza rasmi wikiendi hii kwa kushirikisha wajumbe toka zaidi ya Mabunge ya nchi 150 Duniani.
Msomaji
Thailand

Saturday, March 27, 2010

Rais Kikwete alivyozindua kitabu cha historia ya maisha ya utumishi wa umma ya Sir George Kahama ikulu jijini Dar es salaam

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe ulizingushwa kwenye kitabu kinachohusu historia ya maisha ya utumishi serikalini ya Mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto waoshuhudia uzinduzi huo ni Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin William Mkapa, Mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama(wapili kushoto), Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi(wanne kushoto) na watano kushoto ni Mwandishi wa kitabu hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Royalty Bwana Joseph kahama.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mezani tayari kwa mauzo kitabu kinachohusu maisha ya Mwanasiasa Mkongwe Sir.George Kahama muda mfupi baada ya kukizindua katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin Mkapa, Mwanasiasa mkongwe Sir George Kahama(wapili kushoto) na wanne kushoto ni Joseph Kahama ambaye ni mwandishi wa kitabu hicho. Joseph ni Mtoto wa Mzee Kahama.
Joseph Kahama ambaye ni Mwandishi wa kitabu kinachohusu historia ya Maisha ya Utumishi Serikalini ya Mwanasiasa Mkongwe Sir.George Kahama akimkabidhi Mama Maria Nyerere nakala ya kitabu hicho katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua kitabu hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Joseph Kahama(Wanne kushoto) ambaye ni Mwandishi wa kitabu kinachohusu maisha ya mwanasiasa mkongwe Sir.George Kahama wakati wa hafla ya uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika jijini Dar es Salaam leo jioni.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamim Mkapa, Sir Geroge Kahama(wapili kushoto) na kulia ni Rais Mstaafyu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi
Msomaji
Dar es salaam

Tuesday, March 16, 2010

Nibu waziri Chiza azindua mradi wa kilimo cha umwagiliaji Mwangomole

Naibu Wazri wa maji na Umwagiliaji Christopher Chiza akizindua mradi wa kilimo cha Umwagiliaji wa Mwangomole, katika Kijiji cha Kwala, Kibaha mkoa wa Pwani leo ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa maadhimisho, maadhimisho hayo ya 22 ya wiki ya Maji pia yanafanyika sambamba na maonyesho kwenye viwanja vya Mwendapole.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Christophe3r Chiza (kaundasuti) akiangalia ramani ya mradi huo (anayeamuonesha (katikati ) ni Msimamizi wa Mradi huo Mhandisi, Rogers Ishengoma.
Msomaji
Dar es salaam

Rais Kikwete apokea jezi ua Real Madrid, akabidhiwa pich yake iliyochorwa, na kumpokea waziri mkuu wa Finland Mhe Matti Vanhanen

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mstahiki Adam Kimbisa akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya jezi namba tisa ya Timu ya Real Madrid ya Hispania inayovaliwa na nyota wa timu hiyo Ronaldo ikulu jijini Dar es Salaam leo kwa kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kukuza mchezo wa soka nchini
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu jijini Dar es Salaam Waziri Mkuu wa Finland Matti Vanhanen leo asubuhi baadaye viongozi hao walifanya mazungumzo
Msanii Paul Ndembo ambaye amejikita katika uchoraji wa sura za watu mbalimbali hususan viongozi akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete picha aliyoichora.Msanii huyo alimkabidhi Rais Picha hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijinji Dar es Salaam leo asubuhi. Msanii Paul Ndembo akimuonesha Rais Kikwete moja ya picha alizochora za nyakati mbalimbali za Uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Picha hiyo imewekwa katika ukuta sehemu ya mapokezi ikulu jijini Dar es Salaam.Msanii Paul Ndembo ni Mhitimu katika kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda Mwaka 1970 na ni mchoraji mahiri wa stempu za barua Tanzania
Msomaji
Dar es salaam

Thursday, March 11, 2010

WAZIRI MKUU PINDA KATIKA MKUTANO WA KILIMO NA USINDIKAJI MAZAO ABUJA NIGERIA

Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa na Makamu wa Rais na Kaimu Rais wa Nigeria, Dk. Goodluck Jonathan (katikati) na kushoto ni Rais wa Sierra Leon, Ernest BaiKoroma wakisikiliza wimbo wa taifa wa Nigeria kabla ya kuanza kwa mkutano wa viongozi wakuu wa Afrika kuhusu Maendeleo ya Biashara na Usindikaji wa Mazao yaKilimo uliofanyika kwenye ukumb i wa hoteli ya Transcorp Hilton jijini Abuja
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, Waziri wa Viwanda Biashara na Masoko, Mary Nagu (kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Ali Iddi (kulia) wakitoka kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Transcorp Hilton katika jiji la Abuja baa ya kufungwa kwa mkutano wa viongozi wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Maendeleo ya Biashara na usndikaji wa mazao ya kilimo Machi 10, 2010. Mheshimiwa Pinda alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano huo.
Msomaji
Nigeria

Rais Jakaya Kikwete ziarani Kitunda, Sikonge Mkoani Tabora

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipampu maji kutoka katika kisima kilichonjengwa nawananchi chini mradi unaoratibiwa na shirika la maendelo la umoja wa Mataifa UNDP, katika Kijiji cha Mbola, Wilaynai Uyui, mkoa wa Tabora jana.Anayeangali ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mwakilishi MkaZI wa UNDP Bwana Aberic Kacou.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua ujenzi wa ukarabati wa zahanati ya Kitunda,wilayani Sikonge jana jioni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua shamba la mahindi lililolimwa kwa ubora na mkulima Bwana Abdallah Sebitango Balakekenwa katikA KIJIJI CHA Mbola KAta ya Ilolangulu, Wilayani Uyui, mkoa wa Tabora.Mkulima huyo mwenye kumiliki shamba la ekari 25 ana wake wawili na Rais Kikwete ameahidi kumnunulia ng’ombe wa kulimia ahadi hiyo ilitimizwa hapo hapo
Kikongwe aliyejitambulisha kwa jina la Bi.Zubeti Kungi akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete pamoja na Rais Kikwete muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kuhutubia mkutano wa hadhara, katika eneo la Kitunda, Wilayani Sikonge.Bi Kungi alisema kuwa amezaliwa mwaka 1936 na kuwa alifurahi sana kumuona na kusalimiana na Rais Kikwete pamoja na mkewe.
Msomaji
Tabora

CCM Singida Mjini waaswa kuepuka makundi

KATIBU wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Singida Mjini, Hassan Mazala amewaasa viongozi waandamizi wa Jimbo hilo kuepuka makundi na baadala yake waendeleze mshikamano ilikuendeleza mshikamano na kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao.Akizungumza katika maojiano maalum juu ya hali ya kisiasa jimboni humo, jana jijini Dar es Salaam , alisema kuwa mpaka sasa Viongozi wameweza kutekeleza ilani ya Chama kwa asilimia kubwa na kuendeleza matumaini kwa wananchi, viongozi hao ni Rais, Mbunge na Madiwani katika Halimashauri hiyo ya Manispaa ya Singida.“Viongozi wote waliochaguliwa mwaka 2005 kupitia CCM, wameweza kutekeleza Ilani kwa asilimia kubwa, zikiwemo ahada zao binafsi. hivyo nawaomba Viongozi na wana CCM tuendeleze mshikamano tulio kuwa nao” alisema Mazala.Mazala aliendelea kusema kuwa, kwa kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu, vuiongozi wa wa juu wa Chama ambao ndiyo wanaokuwa na dhamana ya kupendekleza viongozi kuingia katika michakato mbalimbali, aliwaasa kuachana na makundi pamoja na chuki ambapo kama wataepuka hali hiyo Chama kitaendelea kuimalika.“Unaweza kumshagua kiongozi kwa kutumia ulaghai, lakini je anaweza kutekeleza ilani ya Chama kwa vitendo?, hivyo kama viongozi wanajukumu la kuangalia hilo kwa undani na wala wasiangalie wapi kuna maslai binafsi” alimalizia Mazala.

Msomaji
Singida

Luhanjo Maafisa Mipango andaeni sera zinatoa majibu ya matatizo ya wananchi

Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo.
Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo ametoa wito kwa wachumi na maafisa mipango kuandaa sera zitakazosaidia kuondoa matatizo mbalimbali yanayowakabili wananchi wa Tanzania katika kujiletea maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla. Alisema kuwa ni wajibu watendaji hao kuandaa sera nzuri zitakazoweza kutoa majibu juu ya matatizo mbalimbali yaliyopo katika jamii ya Tanzania. Luhanjo alisema hayo jana mjini Morogoro wakati anafungua mkutano wa siku tatu wa Maafisa Mipango na wachumi. Alisema kuwa mipango mizuri ni ile inayojaribu kuondoa changamoto zinazokabili jamii kama vile miundo mbinu mibovu, msongamano wa magari mijini, ongezeko la idadi ya watu lisilolingana na rasilimali zilizopo , magonjwa kama vile malaria, UKIMWI na utegemezi wa bajeti kutoka kwa wafadhili. Luhanjo aliongeza ni vema watendaji wakaanda mipango inayotekeleza kwa kuchagua michache ya kipaumbele kulingana na rasilimali zilizopo ili kufanya mipango hiyo kuwa halisi na inayoleta maenendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Pamoja na kutoa vipaumbele katika mambo machache , Katibu Mkuu Kiongozi pia aliwaagiza Maafisa hao kuzingatia maelekezo yaliyomo katika Dira ya Taifa 2025 na MKUKUTA ili kuwa na mipango mizuri na michache inayotekelezeka. Alisema wakati umefika kwa Maafisa mipango kuandaa mipango mizuri itakayokuwa ukumbusho wa kazi zao na mchango wao kwa Taifa na raia wake. Mkutano huo ni wa nne kufanyika ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu yake ni jukumu la Maafisa Mipango na maendeleo ya uchumi
Msomaji
Morogoro

Wednesday, March 10, 2010

TONY NGOMBALE MWIRU ASIMIKWA KUWA KAMANDA WA VIJANA CCM KATA YA KIJITONYAMA

Mgeni Rasmi na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ridhiwani Kikwete akimsimika Kamada wa Vijana CCM kata ya Kijitonyama kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya msingi Kijitonyama leo jioni makamanda wengine kutoka matawi pia wamesimikwa katika mkutano huo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ridhiwani Kikwete hapa akimvisha ukamada wa Tawil la Bwawani Rehure Nyaulawa.
Ridhiwani Kikwete akifurahia kitu na Mnazi mkubwa wa Simba na Mkereketwa wa Chama Cha Mapinduzi Bw. Kipukuswa mara baada ya kumaliza kazi ya kusimika makamanda wa vijana CCM kata ya Kijitonyama wanaofuatia ni Tony Ngombale Mwiru aliyesimikwa kuwa Kamanda wa Vijana Kata ya Kijitonyama na mwisho ni Rehure Nyaulawa aliyesimikwa kuwa kamanda wa tawi la Bwawani.
Mjumbea wa kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Diwani wa kata ya Kijitonyama Omary Kimbau na Mbunge wa Kinondoni Mh Iddi Azan mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara kwa ajili ya kusimika makamanda wa vijana kata ya Kijitonyama uliofanyika leo katika shule ya mdsingi Kijitonyama.
Mjumbe wa kamati ya Utekekelezaji Umoja wa Vijana CCM Taifa Ridhiwani Kikwete akifungua Tawi la CCM shule ya Kijitonyama katikata nikamanda wa vijana Kata ya Kijitonyama Tony Ngombale Mwiru na kushoto ni Ismail Mwenda katibu Mwenezi CCM tawi la Bwawani.
Wanachama mbalimbali wakifuatilia kila kilichojiri kwenye mkutano huo.
Wanachama mbalimbali wakifuatilia kila kilichojiri kwenye mkutano huo.
Wakereketwa mbalimbali wa chgama cha mapinduzi wakiserebuka na muziki wa taarab wakati makamnda wa vijana wa kata ya Kijitonyama waliposimikwa rasmi jioni leo katika mkutano uliofanyika katika shule ya msingi Kijitonyama.
Msimaji
Dar es salaam

Monday, March 8, 2010

Rais Kikwete Mgeni Rasmi Siku ya wanawake Duniani Kitaifa Mkoani Tabora

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia taifa wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi,Tabora leo mchana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na vikundi mbalimbali vya wanawake wa mkoa wa Tabora wakati alipotembelea mabanda ya maonesho katika viwanja vya Chipukizi mkoani Tabora leo. Umoja wa Wanawake wa UWT wakipita mbele ya Mh. Rais Jakaya Kikwete na wananchi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo mkoani Tabora.
Sehemu ya wakazi wa mji wa Tabora na mikoa mingine ya jirani waliohudhuria kilele cha sherehe ya siku ya Wanawake duniani iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora leo mchana.
Msomaji
Tabora