Dkt. Diodorus Kamala atembelea kiwanda cha East African Cable
Waziri wa Afrika Mashariki Dkt. Diodorus Kamala (wa pili kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Charles Ngachwelwa Meneja ubora wa Kiwanda cha East African Cable kuhusu mtambo wa kutengeneza nyaya za kusukia motor na transfoma wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Joseph Kamau Meneja uzalishaji akifuatiwa na Muriithi Ndegwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda. Waziri huyo alitembelea kiwanda hicho leo kwa lengo la kuona bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo ili aweze kuzitangaza kwa wanachama wa Afrika Mashariki. Waziri wa Afrika Mashariki Dkt. Diodorus Kamala (katikati aliyevaa koti yeupe) akipata maelekezo kutoka kwa Muriithi Ndegwa ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha East African Cable (kulia kwa waziri) kuhusu roll ya waya wa shaba ambayo inaingizwa katika mashine na kutolewa katika ukubwa wa aina tofauti wa nyaya. Kulia ni Charles Ngachwelwa Meneja ubora wa Kiwanda akifuatiwa na Joseph Kamau Meneja wa uzalishaji. Waziri huyo alitembelea kiwanda hicho leo kwa lengo la kuona bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo ili aweze kuzitangaza kwa wanachama wa Afrika Mashariki.
Imani za CCM zimejengwa chini ya misingi ya usawa kwani binadamu wote ni sawa. CCM kinalenga kumuwezesha mwananchi yeyote wa Tanzania kupata maendeleo.
U.S.A.
Contact
Welcome to the blog of CCM members living in the State of Texas in the United States of America. If you'd like more information about CCM, please contact us at ccmtexas12@gmail.com. We welcome suggestions and comments. If you'd like to become a member, email us and we'll assist you as quickly as possible.
What's the most pressing issue for Tanzanians abroad?
No comments:
Post a Comment