Mwenyekiti wa CCM, Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa pili wa SMZ Balozi Seif Iddi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakijadili jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM ilichofanyika ikulu jijini Dar es Salaam
Sunday, March 4, 2012
Kikao cha Kamati Kuu ya CCM
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa pili wa SMZ Balozi Seif Iddi na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakijadili jambo muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM ilichofanyika ikulu jijini Dar es Salaam
Saturday, March 3, 2012
Wednesday, February 29, 2012
Monday, February 27, 2012
CCM orders re-run between Sumari, Sarakikya

Chama Cha Mapinduzi (CCM) yesterday reversed its earlier nomination of a candidate for the Arumeru East by-election and ordered a repeat of the primary polls.The Central Committee, which met at State House under the chairmanship of President Jakaya Kikwete, ordered that the polls be repeated on March 1 on the grounds that none of the aspirants managed more than 50 per cent of the vote as per the party regulations.The CC, which spent eight hours discussing the issue, said the rerun would be between top contenders Sioi Sumari and William Sarakikya. Mr Sumari scooped 361 votes in the primaries and Mr Sarakikya garnered 259. Other contestants, with their votes in brackets, were: Elishilia Kaaya (176), Anthony Musami (22), Elirehema Kaaya (205) and Urio Rishiankira (11).Mr Sumari will now have to battle it out with Mr Sarakikya if he is to succeed his father, the late Jeremiah Sumari.CCM Publicity and Ideology secretary Nape Nnauye told reporters after the meeting that the primaries would be held on March 1 and the results announced a day later. A team of supervisors from CCM headquarters, led by the national vice chairman (Mainland), Mr Pius Msekwa, will oversee the polls. Other members of the team are deputy secretary general (mainland) John Chiligati and Constansia Buhia, a CC member from Kagera Region.After the results of the primaries are announced, the party’s political committee at district and regional level will go through them. The CC will meet again on March 5 to endorse the results.Mr Nnauye defended the CC decision to overrule the results of the primaries as normal practice within the party. “Don’t make this such a special issue,” he said. “As you will recall, in 1995 the CC overruled President Kikwete’s victory against Mr Mkapa (Benjamin).” He also denied claims that Mr Sumari’s victory was overruled due to uncertainty surrounding his nationality. “The CC overruled the primaries results simply because no one got over 50 per cent of the votes as the regulations require and not any other reason,” Mr Nnauye insisted.Mr Sumari told journalists he was happy with the decision since it was aimed at uniting the party ahead of stiff competition from other political parties.He told The Citizen in a telephone interview: “I am okay with the decision since it aims at uniting the party. The votes were very scattered in the previous primaries. I will be content with any results that come out of Thursday’s primaries.” Mr Sarakikya followed up with remarks that he was pleased with the CC decision since it was aimed at getting a candidate who had majority support from party members.Mr Sumari’s victory was received with scepticism by a section of CCM supporters in Arumeru and other parts of the country, with some insinuating that the result was influenced by corruption.As the primaries were being held, several people outside the hall carried placards accusing the party of entertaining corruption in the nomination process. Some posters accused the party of electing leaders on an “inheritance basis”.The senior Sumari died earlier this year. He was serving his second term as Arumeru East legislator after winning in the 2005 election. The by-election will be held on April 1 and is being seen as a two-horse race between CCM and Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Mabadiliko ya Katiba ya CCM

CHAMA Cha Mapinduzi kimefanya mabadiliko ya Katiba yake ya mwaka 1977 toleo la 2010 na kanuni zake, baada ya Halmashauri kuu ya chama hicho chini ya Mwenyekiti wake wa taifa Rais Jakaya Kikwete.Mabadiliko ya katiba ya CCMAkielezea mabadiliko hayo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye anasema, kwanza Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imebadili namna ambavyo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inavyopatikana.“Wajumbe hao waliokuwa wakipatikana kutoka kwenye ngazi ya mikoa, sasa wamegawanywa katika makundi sita ambayo ni ngazi ya Taifa itakayokuwa na wajumbe 10 kutoka Tanzania Bara na wajumbe 10 kutoka Tanzania visiwani” anasema na kuongeza, “Kundi la pili litahusisha wajumbe 10 wa kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM Taifa. Kundi la tatu linahusisha wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao wakati kundi la nne lina wajumbe wanaotoka kwenye vyombo vya uwakilishi kama vile wanaochaguliwa na Bunge nafasi 10 (Bara nafasi nane, Zanzibar nafasi mbili), wanaochaguliwa, Bara tano na Zanzibar nafasi tano)”. Analitaja kundi la tano linalohusisha wajumbe wanaochaguliwa kutoka wilayani nafasi 221. Wajumbe hao waliochaguliwa kupitia wilaya watakuwa ni viongozi wa kazi za muda wote ili kuweka wazi zaidi wajibu wa wajumbe hao wa kuwa karibu na wanachama na kushughulikia shida zao.Kundi la mwisho ni wajumbe toka kwenye jumuiya za chama, kama vile wanaochaguliwa na Umoja wa Wanawake nafasi 15 (Bara nafasi tisa na Zanzibar nafasi sita). “Umoja wa Vijana (UVCCM) nafasi 10 (Bara nafasi sita na Zanzibar nafasi nne). Jumuiya ya Wazazi nafasi tano(Bara nafasi tatu na Zanzibar nafasi mbili)”. Baraza la UshauriKatika mabadiliko hayo Halmashauri kuu ya Taifa imeamua kuwa viongozi wakuu wastaafu ngazi ya taifa waundiwe baraza la ushauri.Nape amesema kuwa, Baraza hilo litakuwa na wajumbe kama vile Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walikuwa wenyeviti wa CCM Taifa. Anawataja wengine kuwa ni pamoja na Marais wastaafu wa Zanzibar ambao pia walikuwa Makamu wenyeviti wa CCM Taifa na Makamu wa mwenyekiti wa CCM Taifa wastaafu.“Baraza litakuwa na kazi ya kutoa ushauri kwa Chama na serikali zinazoongozwa na CCM, kwa madhumuni hayo hayo katika jambo mahsusi. Wajumbe wa baraza hilo wanaweza pia kualikwa ama wote au mwakilishi wao kuhudhuria vikao vya chama ngazi ya Taifa” anasema Nape.Mabadiliko ya Katiba na mbio za urais ndani ya CCMWakati CCM kikifanya mabadiliko hayo, kumekuwa na hofu ya kuwapo kwa mkakati wa kuwadhibiti baadhi ya makada wa chama hicho waliopani kugombea urais mwaka 2015. Hofu hiyo inaelezwa kuwa ni kutokana na kubadilisha namna ya kuwapata wajumbe wa NEC kutoka ngazi ya mikoa hadi wilaya ikiwa ni mkakati wa kuyadhibiti makundi yanayoweza kutumia nguvu ya fedha kuwanunua wajumbe hao kwa malengo yao binafsiJapo chama hicho hakijaanza rasmi mchakato wa kutafuta mgombea urais, tayari baadhi ya makada wametajwa kupita huko na huko ili ‘kujiuza’. Makada hao wameonekana wakipita makanisani na misikitini, wakishiriki ibada na kufanya harambee na matamasha, hali inayotafsiriwa kuwa ni mikakati ya kujitangaza.Baadhi ya makada wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda. Wengine ni pamoja na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Utawala Bora Mathias Chikawe, Waziri wa Ujenzi John Magufuli, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Lazaro Nyalandu na Waziri wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige. Hata hivyo kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanaotajwa wamekanusha vikali kuhusika na mbio hizo. Kati ya waliojitokeza hadharani na kukanusha mikakati hiyo ni pamoja na Samuel Sitta ambaye amesema kama ni urais utamfuata mwenyewe, siyo yeye kuutafuta. Naye Waziri Mkuu Pinda amesema kuwa urais ni mzigo ambao asingependa kuubeba. Naye Lazaro Nyalandu amekanusha si tu kujihusisha na mbio hizo bali hata kushirikiana na wanaokimbilia. Hata hivyo, hofu hiyo imekanushwa na Katibu wa Itikadi na uenezi Nape Nnauye akisema kuwa hakuna sababu ya kuwa na hofu ya kuzuiwa kugombea urais kwasababu tu kushindwa kuingia kwenye NEC. “Sifa ya msingi kwa mtu kugombea urais kwa mujibu wa Katiba yetu, kwanza ni mtu huyo kuwa mwanachama wetu, awe ni mbunge au asiwe,” anasema Nape na kuongeza; “Nimekuwa nikisema mara kwa mara kwamba, hii ni sehemu tu ya mkakati wa kujivua gamba tuliyokuwa tukiitangaza. Hakuna anayelengwa hapa. Yeyote anayedhani kuwa hawezi kugombea urais bila kuwa mjumbe wa NEC, basi hilo ni tatizo na ninaweza kusema kuwa huyo amefilisika kisiasa” anasema Nape. Mbali na kipengele hicho cha kuwapata wajumbe wa NEC, suala la kuunda Baraza la Ushauri linalowahusisha viongozi wastaafu nalo limewekewa alama ya kuuliza kwamba, je, nao ni mkakati mwingine wa kuwadhibiti wagombea urais?Hata hivyo akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni, Nape amesema uundwaji wa Baraza la Ushauri la Wazee umetokana na mawazo ya wazee wenyewe wastaafu wa chama hicho ambao wamebaini ipo haja ya kuwa na chombo hicho kutokana na sababu mbalimbali.“Jambo kubwa ambalo linapotoshwa sana ni la uamuzi wa NEC kuunda Baraza la Ushauri la Wazee. Uamuzi ambao kimsingi ulifikiwa kwenye kikao cha NEC cha mwezi Aprili mwaka 2011 Mjini Dodoma kikao ambacho kiliridhia kufanyika kwa mageuzi ndani ya Chama. Kikao cha February 12, 2012 cha NEC kiliridhia tu mabadiliko ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2010 ili kuruhusu kuundwa kwa baraza hilo,” anasema Nape.Ameongeza kuwa, wazo la kuundwa kwa baraza hilo limetokana na ushauri wa baadhi ya wazee wenyewe wastaafu wakizingatia wingi na urefu wa vikao husika, na si mpango au mkakati wa kuwaengua makusudi wastaafu hao kama inavyodaiwa na baadhi ya wapotoshaji.“Ilikuwa ni ushauri wao kwamba baada ya kustaafu badala ya kulazimika kuhudhuria vikao vya kitaifa kila mara basi wapewe muda wa kupumzika na wanapotakiwa kutoa ushauri watumiwe badala ya utaratibu wa sasa wa kulazimika kuhudhuria vikao ambavyo kwakweli ni vingi na wakati mwingine huisha usiku wa manane,” anasema na kuongeza; “Baada ya wazo la wazee wetu kupumzika, huku tukizingatia kuwa busara zao bado ni muhimu sana kwa Chama na Taifa, busara ikatumika badala ya kupumzika kabisa basi tuunde Baraza la Ushauri la Viongozi wa Kitaifa wastaafu. Na hii haina maana kuwa hawaruhusiwi kuhudhuria vikao vya Chama na kuwa hawatatumika kwa kazi za Chama na Taifa kwa ujumla, isipokuwa mabadiliko haya yanaondoa ulazima wa wao kuhudhuria vikao hivyo kama ilivyokuwa mwanzo.” Pamoja na hayo ameongeza kuwa CCM imebaini chama makini chochote kitatafuta utaratibu bora wa kuwaenzi waasisi wake na kuendelea kuvuna busara na hekima zao katika kuendelea kukijenga Chama. Katika hili CCM imeonyesha mfano mzuri unaostahili kuigwa na vyama vingine. Kuundwa kwa baraza hili na kutambuliwa rasmi na katiba ya Chama ni uthibitisho tosha wa namna CCM inavyothamini wastaafu hawa. “Chama Cha Mapinduzi kinathamini sana busara na mchango wa wastaafu hawa katika ujenzi wa Chama na Taifa kwa ujumla hakiwezi kuwaong’oa au kuwatupa kama inavyojaribu kupotoshwa na baadhi ya watu. Tuwatendee haki wazee wetu hawa badala ya kutumia vibaya majina yao na uamuzi wa Chama ambao una baraka zao,” anasema Nape.
Thursday, February 23, 2012
MH NAPE AELEZEA MABADILIKO YA KATIBA YA CCM
CHAMA Cha Mapinduzi kimefanya mabadiliko ya Katiba yake ya mwaka 1977 toleo la 2010 na kanuni zake, baada ya Halmashauri kuu ya chama hicho chini ya Mwenyekiti wake wa taifa Rais Jakaya Kikwete.Mabadiliko ya katiba ya CCM. Akielezea mabadiliko hayo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye anasema, kwanza Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imebadili namna ambavyo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inavyopatikana.“Wajumbe hao waliokuwa wakipatikana kutoka kwenye ngazi ya mikoa, sasa wamegawanywa katika makundi sita ambayo ni ngazi ya Taifa itakayokuwa na wajumbe 10 kutoka Tanzania Bara na wajumbe 10 kutoka Tanzania visiwani” anasema na kuongeza, “Kundi la pili litahusisha wajumbe 10 wa kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM Taifa. Kundi la tatu linahusisha wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao wakati kundi la nne lina wajumbe wanaotoka kwenye vyombo vya uwakilishi kama vile wanaochaguliwa na Bunge nafasi 10 (Bara nafasi nane, Zanzibar nafasi mbili), wanaochaguliwa, Bara tano na Zanzibar nafasi tano)”. Analitaja kundi la tano linalohusisha wajumbe wanaochaguliwa kutoka wilayani nafasi 221. Wajumbe hao waliochaguliwa kupitia wilaya watakuwa ni viongozi wa kazi za muda wote ili kuweka wazi zaidi wajibu wa wajumbe hao wa kuwa karibu na wanachama na kushughulikia shida zao.Kundi la mwisho ni wajumbe toka kwenye jumuiya za chama, kama vile wanaochaguliwa na Umoja wa Wanawake nafasi 15 (Bara nafasi tisa na Zanzibar nafasi sita). “Umoja wa Vijana (UVCCM) nafasi 10 (Bara nafasi sita na Zanzibar nafasi nne). Jumuiya ya Wazazi nafasi tano(Bara nafasi tatu na Zanzibar nafasi mbili)”. Baraza la UshauriKatika mabadiliko hayo Halmashauri kuu ya Taifa imeamua kuwa viongozi wakuu wastaafu ngazi ya taifa waundiwe baraza la ushauri.Nape amesema kuwa, Baraza hilo litakuwa na wajumbe kama vile Marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao walikuwa wenyeviti wa CCM Taifa. Anawataja wengine kuwa ni pamoja na Marais wastaafu wa Zanzibar ambao pia walikuwa Makamu wenyeviti wa CCM Taifa na Makamu wa mwenyekiti wa CCM Taifa wastaafu.“Baraza litakuwa na kazi ya kutoa ushauri kwa Chama na serikali zinazoongozwa na CCM, kwa madhumuni hayo hayo katika jambo mahsusi. Wajumbe wa baraza hilo wanaweza pia kualikwa ama wote au mwakilishi wao kuhudhuria vikao vya chama ngazi ya Taifa” anasema Nape.
TUIMARISHE CHAMA, TUJITOLEE KWA MOYO WOTE,
Sunday, February 19, 2012
Monday, November 28, 2011
MAKUBALIANO YA RAIS KIKWETE NA UJUMBE WA CHAMA CHA CHADEMA

Ujumbe wa Uongozi wa CHADEMA ukipitia kwa makini taarifa ya pamoja kati ya serikali na chama hicho kabla ya kukisambaza kwenye vyombo vya habari ikiwa ni hitimisho la mkutano wao baada ya mazungumzo ya siku mbili Ikulu jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan wakipitia taarifa hiyo ya pamoja

Sunday, November 27, 2011
MAAMUZI YA KIKAO CHA NEC - CCM

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi iliyokutana kwa siku mbili kuanzia tarehe 23-24 Novemba, 2011 mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mambo mengine imeazimia yafuatayo:
UNUNUZI WA MAHINDI
I. Halmashauri Kuu ya Taifa imeipongeza Serikali kwa kuwa na mkakati wa kutafuta fedha haraka kwa kuamua kuuza mahindi tani 80,000 kwa UNFP na nchini Kenya ili kwanza, kulipa madeni ya wakulima, na pili, kununua mahindi ya wakulima yaliyopo majumbani na kwenye vituo vya ununuzi kabla ya upandaji wa msimu mpya haujaanza.
II. Imeipongeza pia Serikali kwa kuruhusu uuzaji wa mahindi nje ya nchi, hali ambayo itasaidia mahindi yaliyobaki kwa wakulima kupata soko. Hata hivyo, imesisitiza kuwepo na tahadhari sasa na siku zijazo, ili chakula chote kisiuzwe nje ya nchi na kusababisha tatizo la njaa nchini.
III. Imeitaka Serikali iimarishe Wakala wa Chakula wa Taifa kwa kuuwezesha kwa fedha zaidi na kujenga maghala mengi na makubwa zaidi ili uweze kununua kiasi kikubwa cha mazao.
IV. imeiagiza Serikali ihimize kuundwa kwa Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Chakula, ambavyo navyo viwezeshwe kujenga maghala ya kuhifadhi nafaka katika maeneo yao pamoja na kuanzisha mfumo wa ununuzi wa mazao wa stakabadhi ghalani.
MJADALA WA KATIBA
Halmashauri Kuu ya Taifa imewataka wananchi na wanachama wa CCM kuelewa, kutambua, na kuamini kwamba Katiba mpya pamoja na mchakato wa kuipata, ni kwa manufaa ya nchi. Imewataka Wabunge na viongozi wengine wa ngazi zote nchi nzima kuwaelewesha wananchi si tu maudhui yake, bali hata faida zake.
Imeiagiza Serikali, pamoja na/au kupitia Tume ya Kukusanya Maoni, iweke msukumo wa kutoa elimu kwa umma wakati wote kuhusu jambo hili na mchakato mzima ili kuzuia upotoshaji unaofanywa kwa wananchi kuhusu mchakato mzima wa kupata Katiba mpya.
Imeitaka Serikali ihakikishe hakuna Chama chochote cha siasa, mtu, kikundi cha watu au taasisi yoyote ikayotumia mchakato wa kupata Katiba mpya kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani. Vyombo vya Usalama viwe imara katika kuhakikisha kwamba Sheria za nchi zinafuatwa na wanaochochea vurugu wanachukuliwa hatua kali bila kujali nafasi zao.
Aidha, imempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa kwa wazee wa Dar es Salaam kwa ufafanuzi na maelezo fasaha kwa mambo makubwa na ya msingi yanayolikabili taifa letu.
NISHATI YA UMEME NA MAFUTA NCHINI
I. Halmashauri Kuu ya Taifa imeipongeza Serikali kwa kutengeneza mpango wa umeme wa dharura, licha ya gharama kubwa, lakini umesaidia kuleta nafuu katika uzalishaji umeme na kupunguza kero kwa wananchi. imeitaka Serikali kutoa taarifa sahihi kwa wakati kuhusu mgao wa umeme na maeneo yanayoathirika ili kupunguza lawama kwa Serikali.
II. Aidha imeitaka Serikali kuongeza jitihada za kuzalisha umeme kwa vyanzo vingine, hasa makaa ya mawe ambayo yapo nchini na umeme wake ni nafuu.
III. Halmashauri Kuu ya Taifa imepongeza pia jitihada za Serikali kusambaza umeme nchini, ambapo sasa karibu kila Makao Makuu ya Wilaya yana umeme. Hata hivyo, imeitaka Serikali, kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), iongeze kasi ya usambazaji umeme vijijini ili kufikia lengo la Ilani ya Uchaguzi ya CCM la asilimia 30 ya kaya zote nchini kuwa na umeme ifikapo mwaka 2015.
IV. Imepongeza jitihada za Serikali za kutafuta fedha (dola za Kimarekani takriban bilioni 1) za ujenzi wa bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ambalo litawezesha kuongeza uzalishaji wa umeme na kuondokana na matumizi ya mafuta kuzalisha umeme. Aidha, Serikali iharakishe taratibu zote za upatikanaji wa fedha hizo ili utekelezaji wa mradi huo uanze mara moja.
UPANGAJI WA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA.
I. Kutokana na umuhimu wa nishati ya mafuta kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu, Halmashauri Kuu ya Taifa imeitaka Serikali kuhakikisha kwamba EWURA inao uwezo, utaalamu na weledi wa kuisimamia sekta hii ipasavyo. Aidha imeipongeza Serikali kwa uamuzi wa kuwa na hifadhi ya Kimkakati ya Mafuta, na wa kuanzisha Kampuni ya Mafuta ya Taifa kwa sababu itasaidia kuziba pengo pale linapotokea tatizo la hujuma kwa waagizaji wa sekta binafsi.
UCHANGISHAJI FEDHA KWA AJILI YA KUPITISHA BAJETI
Halmashauri Kuu ya Taifa imeipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kuipokea taarifa ya Kamati Teule ya Bunge na kuahidi kuifanyia kazi.
VURUGU KATIKA MIJI NA MAENEO MENGINE NCHINI.
Kumejitokeza wimbi la vurugu katika maeneo mbalimbali hapa nchini hasa katika majiji yetu. Majiji ambayo hivi karibuni yameripotiwa kutokea vurugu zikifanywa zaidi na vijana ni Mwanza, Mbeya na Arusha. Kutokana na hali hiyo, Halmashauri Kuu ya Taifa, imeitaka dola kuchukua hatua thabiti na za haraka kudhibiti vitendo vya hujuma na uharibifu kwa mali za Watanzania. Imesisitiza kuwa Kusiwepo kabisa na uvumilivu kwenye uvunjaji wa amani kwa kisingizio cha kudai haki. Viongozi wa vyama vya siasa wanaojihusisha na vitendo vya uchochezi na hujuma wachukuliwe hatua za kisheria bila kuogopwa.
Hata hivyo, Halamshauri Kuu ya Taifa imeitaka Serikali kuharakisha kutatua matatizo yanayowakabili vijana wa mijini, hususan tatizo la ajira na maeneo ya kufanyia biashara zao ndogo ndogo. Imeitaka kuuangalia upya mfumo wa elimu nchini ili vijana wengi wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne wawe na stadi za ufundi zitakazowapa uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa. Vile vile, mpango wa kujenga shule za ufundi kwenye kila wilaya uliomo kwenye llani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010-2015 utekelezwe haraka.
MIGOGORO VYUO VIKUU NA TAASISI ZA ELIMU YA JUU
I. Halmashauri Kuu ya Taifa imeitaka Serikali ihimize utawala bora katika menejimenti za baadhi ya vyuo vikuu vya umma kama moja ya jawabu la kupunguza malalamiko, migogoro, migomo na vurugu katika baadhi ya vyuo.
II. Imeitaka Serikali kutekeleza Sheria yake ya kupiga marufuku harakati za siasa na uvaaji wa sare za vyama katika maeneo ya vyuo (Campuses). Wafanyakazi wa vyuo na wanavyuo wanaopenda kujihusisha na harakati za siasa basi wafanye hivyo nje ya maeneo ya vyuo. Hii itawafanya jamii ya wanavyuo kutoingilia shughuli za masomo na mipango ya vyuo.
III. Imeiagiza Serikali kuendelea kufuatilia kwa karibu hali ya migogoro na malalamiko hasa katika Chuo Kikuu cha Dodoma na ichukue hatua muafaka kurekebisha hali hiyo.
MIGOGORO YA ARDHI
I. Halmashauri Kuu ya Taifa imeitaka Serikali ihakikishe kwamba katika uwekezaji unaohusisha umiliki wa maeneo makubwa ya ardhi, wananchi wasiporwe au kudhulumiwa au kushurutishwa kuhama kwenye ardhi yao bila fidia stahiki.
II. Iwahamasishe pia wawekezaji waliopewa maeneo ya kulima mashamba makubwa kusaidia wakulima wadogo walio karibu na mashamba hayo makubwa kuinua kilimo chao.
III. Kuhakikisha uongozi wa Serikali katika ngazi zote kushughulikia kwa haraka migogoro ya ardhi nchini ili kupunguza kero kwa wananchi.
IV. Imeipongeza Serikali kwa kushughulikia migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima, ambayo kwa sasa imepungua kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo imesisitiza jitihada ziendelezwe serikali katika kupanga matumizi ya ardhi, hasa kutenga maeneo maalum ya wakulima na wafugaji ili kuepusha muingiliano ambao husababisha migogoro.
KUZAMA KWA MELI YA MV SPICE ISLANDER I TAREHE 10/09/2011
I. Kutokana na maafa yaliyotokea tarehe 10 Septemba, 2011 ya kuzama kwa meli ya Spice Islander I, Halmashauri Kuu ya Taifa imezipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa hatua thabiti na za haraka ilizochukua katika kipindi chote cha maafa na msiba huo na hata baada.
II. Imewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Dr. Ali Mohammed Shein kwa kutoa uongozi thabiti na kuongoza katika kuwafariji na kuwatuliza wananchi wa visiwa vya Zanzibari na Watanzania kwa jumla katika kipindi chote cha msiba huu.
III. Halmashauri Kuu ya Taifa, pia imewashukuru watu binafsi na taasisi mbalimbali zilizoshiriki kwenye zoezi la uokoaji na zilizochangia kwa hali na mali, kwa fedha na vifaa, katika msiba huu. Vilevile, imewashukuru na kuwapongeza wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba waliojitolea kushiriki kwenye zoezi la uokoaji.
IV. Kwa kuwa tayari Tume imeundwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi, Halmashauri Kuu ya Taifa imewataka wananchi wasubiri na waiache ifanye kazi yake kwa uadilifu na kwa muda uliopangwa na kuhakikisha kuwa mapendekezo ya tume hiyo yanafanyiwa kazi.
V. Imeiagiza pia Serikali kuendelea na jitihada zake za kurahisisha usafiri wa abiria kati ya Unguja na Pemba na kati ya visiwa hivyo na Tanzania Bara ikiwemo nia yake ya kununua meli zake.
UTEKELEZAJI WA MAAMUZI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA KUHUSU VIONGOZI WANAOTUHUMIWA.
Halmashauri Kuu ya Taifa baada ya kuyatafsiri maazimio yake 27 ya tarehe 10-11 Aprili 2011, na kupokea taarifa ya utekelezaji wa azimio la “Viongozi wa CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi watafakari, wajipime na kuchukua hatua wenyewe kwa maslahi ya chama, wasipofanya hivyo, chama kiwawajibishe bila kuchelewa”.
Katika kutekeleza sehemu ya pili ya uamuzi huo, Halmashauri Kuu ya Taifa imeiagiza Kamati Kuu pamoja na kamati za siasa za ngazi zote za chama chetu, kupitia kamati za usalama na maadili za ngazi zao, kuanza mara moja mchakato wa kutekeleza azimio hilo kwa mujibu wa kanuni na taratibu zinazohusika za chama, na kwamba zoezi hilo lifanyike bila kuchelewa.
Baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, taarifa za utekelezaji zipelekwe kwenye vikao vya kikatiba vya chama.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Wilson C. Mukama
KATIBU MKUU WA CCM

CCM ipo kila mahali
Nape akutana na wana CCM na watanzania Houston
Katibu wa Itikadi na Uenezi - CCM Taifa Mh. Nape Nnauye akiongea na wanachama wa CCM Tawi la Marekani na watanzania waishio nchini humo huko Houston Texas. Katika ziara hiyo Mh aliaambatana na Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi Ndugu Sixtus Mapunda. Katika mkutano ambao ulifanyika katika ukumbi wa Swiss Royale, Houston. Mh Nape alielezea dhana nzima ya mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo maarufu kama 'kujivua gamba'. Alieleza kuwa kujivua gamba ni muhimu kwa sasa hivi ili kukipa chama sura mpya na mvuto kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla. CCM ni moja kati ya vyama vinne duniani vya kisiasa na kidemokrasia ambavyo vimekuwa madarakani kwa ridhaa ya wananchi kwa muda mrefu, kwa maana hiyo chama makini ni lazima kiendane na wakati ili kiweze kuendelea kupata ridhaa zaidi ya kuongoza. Mh nape aliongeza kwamba, ili chama kipate kasi zaidi ya kutumikia wananchi na kuisimamia serikali yake iliyopo madarakani, Chama Cha Mapinduzi kinajijenga zaidi ndani kwenye Idara zake ili ziweze kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadae.Aidha Mh Nape aliwaasa wana CCM kuwa imara na kuhakikisha kuwa chama kinapata nguvu na mafanikio zaidi na zaidi. Akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa waliohudhuria, Mh Nape alisisitiza kuwa CCM Marekani haina mgogoro wowote wa uongozi na kuwasihi wanachama kutoa ushirikiano kwa viongozi halali wa tawi waliochaguliwa kikatiba.
Kabla ya kumkaribisha Mh Nape, Mwenyekiti wa watanzania waishio Houston Bw. Novatus Simba alimshukuru Mh Nape na ujumbe wake kwa kuweza kufika Houston na kubadilishana mawazo na uzoefu juu ya mambo mbalimbali hasa yale yanayotokea huko nyumbani Tanzania. Bw. Simba, alimwomba Mh. Nape kuwa mara kwa mara apatapo nafasi ya kufika Marekani basi anakaribishwa sana kuzuru Houston na kuongea na watanzania juu ya masuala na mustakabali wa mambo kadhaa yanayotokea huko nyumbani.
Saturday, November 26, 2011
Nape afanya ziara Tawini CCM Marekani

Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Mh Nape Nnauye alifanya ziara ya kikazi nchi Marekani na kutembelea tawi la CCM Marekani mjini Houston.
Katika siku yake ya kwanza Mh Nape aliongea na viongozi wa Tawi katika mkutano wa ndani wa kikazi. Mh Nape alisisitiza umuhimu wa matawi ya nje kuwa mabalozi wazuri wa chama na nchi kwa ujumla. Alilitaka tawi hili kuongeza nguvu na kuwafikia wananchama wengi zaidi ndani ya Marekani. Alitoa wito wa Tawi hili kuwa chachu ya kuongezeka kwa matawi mengine mengi na kuongeza nguvu ya chama ndani ya Marekani. Mh Nape ambaye aliambatana na Katibu Mkuu Msaidizi wa Idara ya Itikadi na Uenezi Ndg. Sixtus Mapunda alitoa rai ya kulitaka tawi la CCM Marekani ambalo lipo Houston, Texas kujiunda kama tawi CCM Texas ili kutoa nafasi kwa matawi mengine kuundwa katika maeneo au majimbo mengine ambayo yanawiana kijiografia ndani ya nchi hii. Alibainisha kuwa ukubwa wa nchi ya Marekani unahitaji maeneo tofauti kuunda matawi kamili ili kufanikisha na kurahisisha shughuli za kichama.
Awali kabla ya kumkaribisha Mh Nape kuongea na viongozi wa tawi, Kaimu Mwenyekiti wa Tawi la CCM Marekani Mh. Amina Lesso alimshukuru Katibu wa itikadi na Uenezi - Taifa pamoja na ujumbe wake kwa kuweza kufika tawini hapa na kuimarisha nguvu za CCM hapa Marekani. Mh Lesso aliomba ziara kama hizi zisiwe mwisho bali ndiyo ziwe zimefungua mlango kwa viongozi wengine wa kitaifa kufika Houston na kutembelea tawi na shughuli zetu za chama.
Mh Nape kesho yake alitarajiwa kufanya mkutano na wanachana na watanzania waishio Houston na maeneo mengine ya jirani.
Safu ya Uongozi wa CCM Tawi la Marekani
Kufuatia matokeo uchaguzi uliofanyika hivi karibuni, Chama Cha Mapinduzi Tawi la Marekani lilipata viongOzi wake wapya kama ifuatavyo:
Mwenyekiti wa Tawi
Ndg. Simon Makangula
Wajumbe wa Halmashauri ya tawi:
Ndg. Amina Lesso
Ndg. Frank Mutafungwa
Ndg. Abdallah Nyangasa
Ndg. Gasper Assenga
Ndg. Isaac Kitogo
Ndg. Caccius Pambamaji
Ndg. Misso Temu
Ndg. Mzee Khalfan
Ndg. Azrat Temu
Aidha Halmashauri ya Tawi ilipokea mapendekezo ya uteuzi wajumbe wa sekretarieti ya halmashauri ya tawi na kufanya uteuzi kama ifuatavyo:
Katibu wa Tawi:
Ndg. Abdallah Nyangasa
Katibu Itikadi na Uenezi:
Ndg. Cassius Pambamaji
Katibu Fedha na Uchumi:

Thursday, May 12, 2011
MABADILIKO YA TAREHE YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI
NDUGU WANACHAMA,
KUTOKANA NA SABABU ZILIZO NJE YA UWEZO WA TAWI, PAMOJA NA KUONGEZA UFANISI WA ZOEZI LA UCHAGUZI, UCHAGUZI WETU UTAFANYIKA TAREHE 12 JUN, KINYUME NA TAREHE 29 MAY, KAMA ILIVYOTANGAZWA HAPO AWALI.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
SALUM RAJABU,
KATIBU WA MIPANGO NA UENEZI WA TAWI,
CCM-MAREKANI

Wednesday, April 27, 2011
TAREHE YA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI
Ndugu Wanachama wa Chama cha mapinduzi,
Ufuatao ni utaratibu wa mwisho katika kukamilisha mchakato mzima wa uchaguzi wa viongozi wa Tawi letu;
Siku ya Mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu za maombi ya uongozi ni Jumapili, Tarehe 8 may 2011.
Na siku ya uchaguzi wa viongozi ni Jumapili, tarehe 22 may 2011.
Tafadhari hakikisha umepata kadi na umelipia ada yako ya mwaka kabla ya siku ya uchaguzi, kwani ni wanachama hai tu watakaoruhusiwa kushiliki katika uchaguzi huu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,
ABDALLAH NYANGASA,
KAIMU KATIBU MKUU
TAWI LA CCM MAREKANI.

Saturday, April 9, 2011
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI LA MAREKANI
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!!
Habari za leo ndugu wanachama,
Wakati muhimu katika kulijenga na kuliendeleza Tawi letu umewadia. Uchaguzi wa viongozi wa Tawi watakaosukuma mbele maendeleo ya tawi na chama chetu umekaribia. Fomu za uchaguzi zitaanza kutolewa leo, zoezi hili la kuchukua na kurudisha fomu litakuwa kwa muda wa wiki mbili kuanzia leo. Tarehe ya uchaguzi itatangazwa ndani ya kipindi hiki cha uchukuaji na urudishaji fomu.
Nafasi zitakazogombewa nikama ifuatavyo:
1. Mwenyekiti wa CCM wa Tawi
2. Wajumbe kumi wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Tawi
3. Katibu wa CCM wa Tawi
4. Katibu wa Siasa na Uenezi wa Tawi
5. Katibu wa Uchumi na Fedha wa Tawi
Ili kuweza kushiliki kikamilifu katika uchaguzi huu kwa kugombea au kupiga kura, hakikisha kwamba una kadi yako ya chama,pia uwe mwanachama hai kwakulipia mchango wa kadi wa kila mwaka kama kadi yako ina muda wa zaidi ya mwaka. Kwa wanaohitaji kadi, kadi zinapatikana kwa kiasi cha $10, na mchango wa kadi wa kila mwaka ili kuwa mwanachama hai ni $25. Malipo yanaweza kufanyika kupitia uongozi wa muda.
Fomu za uchaguzi zipo tayari na zinapatikana kutoka kwa viongozi wa muda kupitia njia za mawasiliano hapo chini ya habari hii.
Anwani ya muda:
7447 Harwin drive ste 220B, Houston, TX 77036.
Namba za simu za viongozi wa muda wa Tawi:
Novastus Simba – Mwenyekiti 832-208-8344
Abdalla Nyangasa – Katibu Mkuu 832-537-11694
Misso Temu - Katibu wa Uchumi na Fedha 281-995-0019
Salum Rajabu – Katibu muenezi wa Tawi 832-524-9608
Salum Rajabu
Katibu wa Siasa na Uenezi wa Tawi

Subscribe to:
Posts (Atom)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernard Membe (kati) akiwa na maafisa wa serikali wakipitia taarifa hiyo