
Monday, August 31, 2009
UONGOZI WA CCM - MAREKANI WAKUTANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI.

Uandikishaji wapiga Kura Pemba!!
Msomaji
Zanzibar
Friday, August 28, 2009
Vigogo wawili miundombinu waondolewa katika nyadhifa zao

Wiki hii Rais Jakaya Kikwete, aliidhinisha mabadiliko ya muundo wa Wizara ya Miundombinu, ikiwemo kuanzishwa Idara mpya ya Miundombinu ya Usafiri inayojumuisha usimamizi wa Reli na Bandari.
Kwa mujibu wa muundo huo mpya, aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchukuzi, Dk Bathlomew Rufunjo, ameondolewa katika nafasi hiyo.
Idara hiyo sasa inaitwa ya Huduma za Uchukuzi ambayo inaongozwa na Dk William Nshama, ambaye alikuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Msemaji Mkuu wa Wizara hiyo Patrick Ntemo, alipoulizwa jana, alisema mabadiliko tayari yalizungumzwa na Katibu Mkuu, Mhandisi Omari Chambo , hivyo hana la kusema.
Hata hivyo, duru nyingine za habari ziliweka bayana kwamba, Dk Rufunjo huenda akapangiwa kazi nyingine.
Katika muundo huo, Elius Mwakalinga ambaye alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Nyumba, naye anasubiri ama kupangiwa kazi nyingine.
Akitangaza muundo huo, Katibu Mkuu Mhandisi Chambo, alisema Idara ya Huduma za Ufundi na Umeme itakuwa na sehemu za Ufundi na Umeme na Majengo ya umma.
Idhini hiyo ya rais imekuja katika kipindi ambacho wizara hiyo imekuwa ikiweka mipango ya kupatia ufumbuzi matatizo makuu ikiwemo ya Shirika la Reli (TRL), Bandari na usimamizi wa majengo ya serikali.
Katibu Mkuu Chambo, alifafanua kwamba, lengo la muundo huo ni kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi wa wizara.
Msomaji
Dar es salaam
Thursday, August 27, 2009
SERIKALI YAKANUSHA MADAI YA TBC KUUZWA

Serikali imekanusha madai ya shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuuzwa kinyemela kama ilivyoonyeshwa katika taarifa iliyotolewa na chombo kimoja cha habari hapa nchini.Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar esa Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu hatua iliyochukuliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuunda kampuni mpya iitwayo Star Media (Tanzania) Limited kwa ubia na mwekezaji.
Amesema Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kama shirika la umma halijauzwa na kuwataka wananchi kutoamini taarifa zozote zinazotolewa kuhusu kuuzwa kwa namna yoyote kwa shirika hilo.
“ Nawathibitishieni leo kuwa shirika la Utangazaji (TBC) halijauzwa ,bado ni la wananchi na kamwe halitauzwa” amesisitiza.Ameongeza kuwa TBC ni mali ya umma na itaendelea kuwa hivyo kama shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na kuongeza kuwa Star Media Tanzania Limited ni Kampuni tanzu ya TBC.
Amefafanua kuwa TBC imeunda kampuni hiyo mpya kwa ubia na mwekezaji aliyeteuliwa kihalali ili kutekeleza mabadiliko ya Digitali na kuendesha mitambo ya kurushia matangazo yake nchi nzima kazi ambayo itakamilika mwaka 2012 kwa gharama ambazo TBC isingeweza kuzimudu yenyewe kutokana na jukumu hilo kuhitaji utaalam mkubwa wa kiufundi ili kukamilisha ufanisi.
Msomaji
Dar es salaam
Wednesday, August 26, 2009
Rais Kikwete alivyoshiriki Mazishi ya Askofu Antony Mayala
Msomaji
Dar es salaam
Maadhimisho ya JWTZ kutimiza miaka 45 ilivyofana
Monday, August 24, 2009
Kura Za Maoni !!
WAISLAMU NCHINI WATAKIWA KUACHA MAOVU

Waislamu nchini wametakiwa kutenda matendo yaliyo mema na kujiepusha na maovu katika maisha yao ili waweze kupata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wito huo umetolewa hivi karibuni na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya wakati akiongea na Waislamu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kongamano la kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani lililofanyika viwanja vya Mnazi Mmmoja.
Waziri Kapuya ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika kongamano hilo aliwataka waislamu hao pia kufuata nguzo tano za imani yao ambazo ni kutoa shahada, kusimamisha swala, kufunga mwezi wa Ramadhani, kutoa zaka na kwenda kuhiji Makka kwa wale wenye uwezo.
"Watukufu Waislamu ninachosema hapa ni kwamba binadamu ameumbwa, ataishi, atakufa, atafufuka, atahukumiwa na baada ya hapo ataishi katika raha au mateso kutokana na vitendo vyake hapa Duniani hivyo basi ni wajibu wenu kuishi kadri ya neno la Mungu linavyosema", alisema.
Akiongelea umuhimu wa kufunga wakati wa Mwezi wa Ramadhani Waziri Kapuya alisema kuwa kufunga ni amri na lazima kwa kila muislamu kama Mwenyezi Mungu anavyosema katika aya ya 183 ya Surat Al-Bakara.
Msomaji
Dar es salaam
Wahanga wa mabomu Mbagala Walipwa !!
Thursday, August 20, 2009
KONGAMANO LA KUJADILI ATHARI ZA UANDIKISHWAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA PEMBA LAENDELEA JIJINI!
Viongozi na wadau mabalimabli wa siasa wakiwemo wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanahudhuria Kongamano hilo, ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa wajumbe na kujadiliwa katika kongamano hilo na kutolewa mapendekezo ya hatua zitakazochukuliwa , kutoka kulia ni Waziri Mkuu wa zamani Joseph Sinde Warioba, Katibu Mkuu wa chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ,Katibu mkuu wa Zamani wa AU amabyo zamani ilijulikana kama OAU Salim A. Salim na Mwenyekiti wa Chama hicho Prf. Ibrahim Lipumba.
Msomaji
Dar es salaam
NAIBU WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR ALLY J.SHAMHUNA ATEMBELEA TSN
Msomaji
Tuesday, August 18, 2009
EVANCE MHANDO WA TBC1 AKIZUNGUMZA NA HASHEEM THABEET.

Pamoja na yote Hasheem aliwataka vijana wa Kitanzania kujitahidi kwenye michezo pia na kutilia mkazo suala la Elimu na kutokata tamaa mapema kwenye kila jambo wanalolitaka katika Maisha yao.
Msomaji
Dar es salaam
Thursday, August 13, 2009
Hospitali ya Ludewa !!
Msomaji
Mbeya
Wednesday, August 12, 2009
Tanzania to Spend $5 Billion on Transport Upgrade
Tanzania will spend $5 billion over the next five years to upgrade its transport system, Infrastructure Development Minister Shukuru Kawambwa said.
The project is part of the East African nation’s transport investment program, which will run over two five-year phases and will develop roads, ports, railways, airports and ferries, Kawambwa said at a conference in the commercial capital Dar es Salaam today.
“It is expected that by 2018, all trunk roads will be paved, thus enabling all regional centers to be linked with paved roads and all district headquarters to be linked with all weather roads,” he said.
Due to low levels of investment, Tanzania’s transport infrastructure is inadequate to cope with growing demand, Kawambwa said.
The government can “ill afford” to develop the system alone, and needs to partner with the private investors, he said, without adding more detail.
The country is in talks with the Japanese government to secure funds to build flyovers in Dar es Salaam to ease traffic congestion, Prime Minister Mizengo Pinda said on July 27.
Msomaji
Dar es salaam
The project is part of the East African nation’s transport investment program, which will run over two five-year phases and will develop roads, ports, railways, airports and ferries, Kawambwa said at a conference in the commercial capital Dar es Salaam today.
“It is expected that by 2018, all trunk roads will be paved, thus enabling all regional centers to be linked with paved roads and all district headquarters to be linked with all weather roads,” he said.
Due to low levels of investment, Tanzania’s transport infrastructure is inadequate to cope with growing demand, Kawambwa said.
The government can “ill afford” to develop the system alone, and needs to partner with the private investors, he said, without adding more detail.
The country is in talks with the Japanese government to secure funds to build flyovers in Dar es Salaam to ease traffic congestion, Prime Minister Mizengo Pinda said on July 27.
Msomaji
Dar es salaam
Tanzania to Halt Power Utility’s 41-Year Monopoly by Year-End

Tanzania plans to enact a law allowing private companies to provide electricity in the East African nation by the end of the year, halting a four decade- long monopoly held by the Tanzania Electric Supply Company Ltd.
Tanzania will publish the Electricity Act, which enables other providers to generate power, in the government gazette by year-end, Deputy Energy Minister Adam Malima said on the sidelines of a conference in the commercial capital Dar es Salaam today.
“The private sector is more than welcome to invest by doing it alone or by partnering with the public sector,” Energy Minister William Ngeleja said at the convention.
Tanzania suffers from recurring power shortages due to insufficient investment in its electricity-generating capacity. The government approved a 300 billion-shilling loan for the state-owned power utility, known as Tanesco, to help it upgrade its infrastructure, Ngeleja said. The funds form part of a 1.95 trillion-shilling recovery plan announced in June, with the World Bank and Millennium Challenge Corp. contributing to the project.
Ngeleja said the government “was aware” of barriers which deter private capital from the industry and that it was changing its power-industry reform plan, first released in 1999, to make it more conducive to investment, he said
Msomaji
Dar es salaam
Tuesday, August 11, 2009
SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA UUZAJI WA MAGOGO NJE YA NCHI
Serikali imewataka wafanyabishara wa mazao ya misitu kuwekeza hapa nchini kwa kujenga viwanda vitakavyosaidia kukuza ajira na kuongeza pato la taifa badala ya kukimbilia kuuza mazao ya misitu hususan magogo nje ya nchi kinyume cha sheria. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Felician Kilahama wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi kuhusu madai ya usafirishaji wa magogo nje ya nchi.
Dk. Kilahama amesema sheria Misitu ya Tanzania Namba 14 ya mwaka 2002 ambayo ilianza kutumika rasmi Julai 2004 inazuia na kupiga marufuku uuzaji na biashara ya aina yoyote ya magogo nje ya nchi.“Sheria yetu ya mwaka 2002 iliyoanza kutumika Julai 2004 hairuhusu kwa namna yoyote kufanyika kwa biashara ya magogo nje ya nci na anayeuza magogo na rasilimali za misitu nje ya nchi ni mwizi, rasilimali ya misitu imehifadhiwa kisheria na ipo kwa ajili ya watanzania” Amesema.
Tanga kwenda Morogoro bali tunazuia wale wasiolipia ushuru na kukiuka masharti na leseni za biashara” Aliendelea kufafanua Dkt. Kilahama. Akitoa taarifa za baadhi ya matukio ya uharibifu wa misitu hapa nchini Dk. Kilahama amesema bado kuna wananchi ambao wanaendelea kufanya biashara ya magogo kinyume cha sheria akiitaja baadhi ya mikoa hapa nchini kama Rukwa, Kigoma ,Ruvuma, Tabora na Pwani kuwa wananchi walio wengi hawana uelewa wa kutosha wa utunzaji wa misitu.
Msomaji
Dar es salaam
Mazishi ya makamu wa rais wa Zimbabwe Mrehemu Joseph Wilfred Msika
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Ali Mohamed Shein akimfariji Mjane wa Marehemu wa Makamu wa Rais wa Zimbabwe Mama Mai Maria Msika wakati alipomtembelea nyumabni kwake nje kidogo ya Mji wa Harare kutoa salamu za ploe kufuatia kifo cha Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joseph Wilfred Msika. Katikati ni Mama Mwanamwema Shein.
Msomaji
Monday, August 10, 2009
Taifa Stars itaelekea Rwanda.
Msomaji
Dar es salaam
Saturday, August 8, 2009
MAMA SALMA KIKWETE ALIVYOPEWA ZAWADI NA MWAKILISHI WA UNICEF
Laakkonen pamoja na Makamishina wenzake walitembelea ofisi za WAMA kwa ajili ya kutoa mrejesho wa shughuli ya ziara yao ya wiki moja waliyoifanya hapa nchini baada ya kupata mwaliko kutoka wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto.
Msomaji
Dar es salaam
Friday, August 7, 2009
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI WILLIAM NGELLEJA AKIFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI
Msomaji
Tuesday, August 4, 2009
N. Korea says 2 U.S. journalists will be freed
Announcement of pardon comes after Bill Clinton meets with Kim Jong Il

North Korean leader Kim Jong Il has pardoned two jailed American journalists and ordered their release following an unannounced meeting with former President Bill Clinton, the North's state media said Wednesday.
The release of Laura Ling and Euna Lee was a sign of North Korea's "humanitarian and peace-loving policy," the Korean Central News Agency reported.
Clinton met with the reclusive and ailing Kim on Tuesday, shortly after landing in the capital Pyongyang. It was Kim's first meeting with a prominent Western figure since his reported stroke nearly a year ago.
SEOUL,
South Korea
Rais Kikwete azindua ujenzi wa barabara ya Singida-Minjingu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omari Chambo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi huo litawekwa na Rais Jakaya Kikwete.
Alisema ujenzi wa barabara hiyo umegawanywa katika awamu tatu. Awamu ya kwanza ya Singida- Katesh ina urefu wa kilomita 65, Katesh- Dareda kilomita 74 na Dareda Minjingu kilomita 85.
Alisema kuwa ujenzi huo wa barabara ya lami unagharamiwa na serikali kuu kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya maendeleo ya Afrika (ADB). Ujenzi huo utakamilika ndani ya miezi 33.
Aidha, Chambo amewataka makandarasi waliopewa zabuni ya ujenzi wa barabara hiyo kuzingatia masharti yote muhimu yaliyomo kwenye mkataba ikiwemo kumaliza kazi kwa wakati.
Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili hapa jana jioni kwa ziara ya siku tatu ambapo atazindua miradi mbalimbali ya mendeleo ikiwemo kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara hiyo.
Msomaji
Singida
Rais Kikwete Ashauri Watanzania Kununua Matrekta Badala Magari Ya Anasa

Rais Kikwete alitaja sababu zingine zinazofanya kilimo kisifanikiwe kuwa ni pamoja na ukosefu wa wataalamu wa kufanya utafiti katika sekta ya kilimo
“Watafiti wengi wanaamini kuwa mbegu nzuri ya kupandwa ni ile iliyozalishwa katika maeneo husika sio ya kuagiza kutoka nje, sasa sisi tunaagiza nje asilimia 75 ya mbegu bora zote tunazopanda hapa nchini hiyo ni hatari kwetu” alisema Kikwete.
Katika maonyesho hayo ambayo kaulimbiu yake ni ‘Kilimo kwanza’Mapinduzi ya kijana uhakika wa chakula na kipato,rais alisema haiwezekani kukosa chakula kila mwaka kana kwamba Watanzania wamelaaniwa.
Alisema kila mwaka Tanzania imekuwa ikikosa chakula wakati ardhi ya kutosha ipo pamoja na baadhi ya maeneo kuwa na mvua za uhakika kitu ambacho ni ndoto katika maeneo ya nchi nyingine duniani lakini bado wanazalisha chakula cha kutosha.
Hata hivyo aliponda kwa Watanzania kuendelea kutumia jembe la mkono na akasema kuwa hicho ni kikwazo kingine cha kuwafanya waendelee kubaki katika hali ya umasikini mkubwa ambao utaendelea kuisumbua nchi.
Pamoja na kusema kuwa kilimo cha jembe la mkono kimepitwa na wakati, aliwaacha hoi wakulima pale aliposema kuwa hata kilimo cha jembe la kukokotwa na ng’ombe ni cha zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
“Sisi tunahimiza kilimo cha jembe la kukokotwa na wanyama huku tukisahahu kuwa kilimo hicho kilikuwepo tangu hata kabla ya Yesu Kristo kuzaliwa ambayo ni zaidi ya miaka 2000 iliyopita, lakini sisi ndio kwanza tunaanza”
Katika hatua nyingine rais Kikwete amesema Benki ya Wakulima nchini itaanzishwa kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya China na tajiri maarufu wa Kimarekani Bill Gates.
Rais Kikwete alisema, mkakati huo umekuja kutoka na ukosefu wa vyombo vya fedha vya uhakika vya kutoa mitaji kwa wakulima hapa nchini.
Kikwete alisema serikali imeamua kuchukua hatua hiyo kwa kuwa ukosefu wa mitaji kwa wakulima umekuwa ni kikwazo kikubwa kinarudisha nyuma maendeleo ya kilimo nchini.
Aliongeza kuwa wakulima wengi hawana uwezo wa kununua matrekta kutokana na kuuzwa kwa bei ya juu pamoja na serikali kuondoa kodi kwenye nyenzo hiyo ya kilimo.
“Serikali iligundua uwezo mdogo wa wakulima kununua matreka.Pamoja na kuondoa kodi katika matrekta ili kuwasaidia wakulima lakini bei bado iko juu” alisema Rais Kikwete.
Habari hii imeandaliwa na Habel Chidawali, Patricia Kimelemeta,Dodoma na Hussein Kauli, Dar
Msomaji
Dodoma
UNHCR YAKABIDHI MAGARI NA PIKIPIKI KWA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Msomaji
Dar es salaam
Subscribe to:
Posts (Atom)